Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Saturday, May 4, 2013

YALIYOMPATA RICK ROSS, SASA YAMPATA WEEZY. MKATABA WAKE NA MOUNTAIN DEW WAPIGWA CHINI

Baada ya Rick Ross kupigwa chini na Reebook, sasa ni zamu ya Tunechi. Lil’ Wayne amepoteza mkataba wake kama msemaji wa kinywaji cha Mountain Dew kufuatia mashairi kwenye wimbo wake Karate Chop.
lilwayne_emmett_till
Lil’ Wayne ambaye amekuwa akitumiwa kwenye matangazo ya Mountain Dew tangu mwaka 2012, ameikasirisha familia ya Emmitt Till kwenye wimbo “Karate Chop” ambapo Weezy anasikika akisema, “Pop a lot of pain pills, ’bout to put rims on my skateboard wheels … beat that p***y up like Emmett Till.”
Emmett Louis Till alikuwa ni mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyeuawa huko Mississippi mwaka 1955 akiwa na miaka 14 baada ya kumtongoza msichana wa kizungu.
Licha ya kutuma barua ya kuomba radhi kwenye familia hiyo, ilikataliwa na ndugu zake pamoja umma kumkosoa vikali Lil Wayne.
Japo kampuni ya Pepsi haijatoa maelezo zaidi, hatua hiyo ilitangazwa na msemaji wa Lil Wayne Sarah Cunningham, aliyesema kuwa ni kutokana na kupishana kiubunifu.

0 comments:

Post a Comment