Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Saturday, May 4, 2013

Azam FC washindwa kuendeleza rekodi yao kwenye kombe la shirikisho,wafa kiume watolewa kwa mabao 2-1 na AS FAR Rabat ya Morocco

Azam fc wakiwa wakishiriki kwa mara ya kwanza katika kombe la shirikisho wametolewa katika hatua ya 3 katika michuano hiyo kufuatia kupokea kichapo cha goli 2-1 toka kwa timu yenye uzoefu AS FAR Rabat ya Morocco.Azam wakiwa wageni wa AS FAR Rabat waliuwanza mchezo taratibu huku AS FAR Rabat wakifanikiwa kutia mpira kwenye nyavu za Mwadini Ally katika dakika ya 1 lakini goli hilo lilikataliwa kutokana na mchezaji aliyedumbukiza mpira nyavuni kuwa ameotea.

John Raphael Bocco aliwanyamazisha mashabiki wa AS FAR kufuatia goli alilofunga katika dakika ya 6 kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Bocco na mpira kuingia moja kwa moja katika nyavu za AS FAR.
Goli hilo lilipelekea AS FAR Rabat kuendelea kutawala mchezo na mnamo dakika ya 12 Rabat walipata goli la kusawazisha kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Abdul-halim Ash-shakir.
Azam fc waliendelea kutumia mashambulizi ya kushtukiza na kupoteza nafasi kadhaa, na katika dakika ya 34 mfungaji wa goli la Rabat Abdul-halim Ash-shakir alizawadiwa kadi nyekundu na kupeleka utawala wa mchezo kwa azam fc.
Kadi nyekundu hiyo ya moja kwa moja kwa Ash-shakiri kufuatia mchezaji kucheza faulo mbaya kwa Brian Umonyi.
AS FAR Rabat walijipatia goli la pili katika dakika 42 kupitia kwa Mohammed Altadir na kuwafanya kwenda Azam fc mapumziko wakiwa nyuma kwa goli 2-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku azam fc wakiendelea kupoteza nafasi na mnamo dakika ya 55 Azam fc walipata pigo kufuatia David Mwantika kuzawadiwa kadi nyekundu, na katika dakika ya 75 Waziri Salum pia kuzawadiwa kadi nyekundu.
John Bocco amanusura aipeleke azam katika hatua inayofuatia baada ya kupoteza penati katika dakika ya 82 na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam fc kuchapwa goli 2-1.

Azam fc leo:
MWADINI ALLY, HIMID MAO, WAZIRI SALUM (Kadi nyekundu 75), DAVID MWANTIKA (kadi nyekundu 55), JACKSON ATUDO, MICHAEL BOLOU, BRIAN UMONYI / KHAMISI MCHA, SALUM ABOUBAKARI, HUMPHREY MIENO / MWAIKIMBA, JOHN BOCCO, KIPRE TCHETCHE.       

0 comments:

Post a Comment