Meneja Mkuu wa kampuni ya Tigo, Diego
Gutierrez( kushoto) akizindua INTANETI YA HARAKA ZAIDI TANZANIA, huduma
ya intaneti ya 4G, ambayo ni huduma yenye nguvu zaidi ya vipimo vya
hadi 42Mbps itakayowawezesha wateja hao kuperuzi, kupakua na kupakia
taarifa mbalimbali kwenye mtandao na kucheza gem kwa haraka zaidi kuliko
ilivyokuwa siku za nyuma.Kulia Deon Geyser mfanyakazi kutoka Tigo.
Uzinduzi huo umefanyika kupitia
teknologia ya mikutano kwa njia ya mtandao yaani ‘video skype’
iliyounganisha mikoa 4 kwa hotuba maalum iliyokuwa ikitolewa na Ndg.
Gutierrez kutoka ofisini kwake makao makuu ya kampuni ya tigo Dar Es
Salaam.Mikoa shiriki katika uzindizi huo pamoja na Dar Es Salaam ni
Dodoma, Arusha na Morogoro.
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam akimuuliza swali Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania wakati wa uzinduzi huo.
Mwakilishi kutoka kampuni ya Tigo,J
OHN SICIMILA (kulia) akimkabidhi William Mganga (katikati) Mshindi wa
Samsung S3 phone kupitia ‘raffle droo’ iliyo fanyika katika chuo kikuu
cha Dar es Salaam. Kulia ni Lilian Matari msaidizi wa uandaaji wa zoezi
hilo.
Waandishi wa habari wa chuo kikuu cha
Dar es Salaam wakicheza michezo kwenye Playstation 3 na Waandishi wa
habari kutoka Dodoma kupitia kasi mpya ya Intanet ya Tigo yenye ubora
nchi nzima.
Mwakilishi kutoka kampuni ya Tigo,
JOHN SICIMILA akikabidhi modem mpya za Tigo mmoja wa washindi
walioshinda katika michezo ya Playstation 3 kati ya chuo cha DSM na
Dodoma.
Waandishi wa habari walipata fursa ya
kuzungumza moja kwa moja na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzanua Ndg. Guiterrez
na maofisa wengine wa Tigo kutoka mikoa hiyo shiriki 4 waliopata fursa
ya kutoa maoni yao.
Kuanzia leo wateja wa tigo wataanza
kufurahia huduma ya intaneti ya 4G, ambayo ni huduma yenye nguvu zaidi
ya vipimo vya hadi 42Mbps itakayowawezesha wateja hao kuperuzi, kupakua
na kupakia taarifa mbalimbali kwenye mtandao na kucheza gem kwa haraka
zaidi kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.
Meneja mkuu wa tigo Ndg. Diego
Gutierrez anasema, “Tunatambua shauku kubwa ya wateja wetu katika kupata
huduma iliyobora na ya haraka zaidi ya intaneti, nasi tunajitahidi
kadri tuwezavyo, kukidhi kiu yao kwa kuwapatia huduma bora na kwa
gharama nafuu zaidi kadri inavyowezekana. Uzinduzi huu ni sehemu tu ya
mpango mkakati wetu wa kuboresha mtandao wetu”.
Huduma za kiganjani za intaneti kwa
makampuni ya simu ni moja ya huduma muhimu zaidi katika soko la mitandao
hiyo na kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), watumiaji
wa intaneti Tanzania hadi sasa wanakisiwa kufikia watu milioni 5.
“Kuingiza sokoni kwa vipimo vya
42Mpbs ‘super fast internet speed’ ni ushahidi tosha wa juhudi za tigo
za kuongoza makampuni mengine ya simu kwa kuwapatia wateja wetu huduma
bora zaidi na za kutosheleza,” alihitimisha Ndg.Gutierrez.
Uzinduzi huo umefanyika kupitia
teknologia ya mikutano kwa njia ya mtandao yaani ‘video skype’
iliyounganisha mikoa 4 kwa hotuba maalum iliyokuwa ikitolewa na Ndg.
Gutierrez kutoka oficini kwake makao makuu ya kampuni ya tigo Dar Es
Salaam. Waandishi wa habari nao walipata fursa ya kuzungumza moja kwa
moja na Ndg. Guiterrez na maofisa wengine wa tigo kutoka mikoa hiyo
shiriki 4 waliopata fursa ya kutoa maoni yao. Mikoa shiriki katika
uzindizi huo ni pamoja na Dar Es Salaam, Dodoma Arusha na Morogoro
Mkutano huo wa waandishi wa habari
ulifuatiwa na mashindano ya michezo kwa njia ya mtandao kati ya
wanafunzi wa vyuo vikuu viwili nchini Tanzania ambavyo ni Chuo Kikuu Cha
Dar Es Salaam na Chuo Kikuu Cha Dodoma ambapo wasomi hao walishindana
katika michezo maarufu ya FIFA na ule wa mbio za magari huku washindi
wakizawadiwa simu za kisasa za ‘smart phone’ na modemu za spidi kubwa za
tigo.
0 comments:
Post a Comment