Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Thursday, May 30, 2013

Ombaomba feki akamatwa mjini Iringa,soma story nzima hapa...

WAKAZI wa mjini Iringa hivi karibuni
wameshuhudia kituko cha mwaka baada ya
kumnasa mzee mmoja akijifanya ombaomba
kwa kuigiza ulemavu asiokuwa nao.
Ombaomba huyo feki alijifanya hana mkono
wa kushoto na mguu wa kulia na kuweka pozi
la kuomba kama vile ni mlemavu katika eneo
la Hazina Ndogo, mjini hapa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,
mlemavu huyo feki ameumbuliwa na mtu
mmoja ambaye alimuona asubuhi ya siku ya
tukio akiwa hana ulemavu wowote kabla ya
kumkuta mchana akiomba kwa kujifanya ni
mlemavu wa mkono na mguu.
Mtu huyo aliwaambia baadhi ya wananchi siri
ya ombaomba huyo na kuwafanya kupandwa
na hasira na kuanza kumshushia kipigo
wakitaka kuhakikisha kama kweli ni mzima
kiasi cha kumuumiza usoni.
Kwa hofu ya kuuawa, mlemavu huyo feki
alijinusuru kwa kuonesha mkono wake wa
kushoto aliokuwa ameuficha ndani ya koti
alilolivaa na mguu aliokuwa ameukunja na
kuukalia.
Wakati wananchi wenye hasira wakiendelea
kumpiga, mzee huyo alijitahidi kupata upenyo
na kutimua mbio ndefu kukimbilia eneo la
Miyomboni na kuwaacha watu wengine wakiwa
hawana mbavu kwa vicheko.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
walipoongea na mwandishi wetu walisema
wakati mwingine ombaomba huyo hujifanya
bubu na kuwaomba watu fedha za matibabu.
Inadaiwa kuwa hii si mara ya kwanza kwa
ombaomba huyo kushtukiwa akifanya mchezo
huo, awali alishawahi kufukuzwa katika
Kitongoji cha Santoni mjini hapa.
“Bahati yake amekimbia kama tukimkuta tena
akijidai ni mlemavu tutamvunja mkono na
mguu ili awe mlemavu kweli,” alisema mmoja
wa mashuhuda wa tukio hilo.
Tuhuma nyingine zinasema kuwa ombaomba
huyo hutumia mbinu hizo za kitapeli kwa
kuwa amekimbiwa na mpenzi kutokana na
kutokuwa na kipato.
Wananchi hao wenye hasira wameutaka
uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana
ombaomba wote wanatumia udanganyifu
kujipatia fedha na kutaka kuwepo kwa
utaratibu maalum wa kuwasaidia wanaohitaji
misaada ya kweli.

0 comments:

Post a Comment