Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Thursday, May 16, 2013

HUYU NDIE SISTER ' FEKI' RAIA WA KENYA ALIYEKAMATWA KWA UTAPELI IRINGA


Mwanamke - anayejiita Sister Phylis Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini Kenya akiwa ofisi za kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada ya kukamatwa.
Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.

.....................................................................................


MAANDIKO matatatifu ya kibiblia yanasema kuwa siku za mwisho yatatokea mambo mengi ya kushangaza dunia ,kamwe kama dalili za siku za mwisho basi naweza kusema ndizo hizi kwani kila kukicha ni mambo mapya ya kushangaza .

Wakati Taifa likiwa katika maswali yasiyo na majibu juu ya tukio la bomu kuua Kanisani mkoani Arusha ,mkoani Iringa mwanamke mmoja anayetambulika kwa Phylis Wanjiru ( 44)raia wa Kitui nchini Kenya amekamatwa akitaka kuwatapeli Masister wenzake .

Mwanamke huyo akiwa amevalia ya kitawa mfano wa masister wa kanisa Kathoriki alikamatwa na kufanyiwa upekuzi na kukutwa na baadhi ya vielelezo vilivyothibitisha utapeli wake huo .

Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi baada ya masister wenzie kubaini kama si mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya masuala ambayo ni msingi wa utawa wao. 

Taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa zinaeleza kuwa mwanamke huyo kabila lake ni Muwembu wa nchini Kenya amekamatwa katika nyumba za masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.

Hata hivyo mwanamke huyo ambaye awali aligoma kutoa maelezo ya kina juu ya ujio wake nchini Tanzania, katika upekuzi walimkuta na baadhi ya chip (Line) za makampuni mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya nchi.

Sister huyo feki alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa niya Africa Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa na jumuiya ya Kenya namba A. 1790366.

Amesema Sister huyo feki katika hati hizo ilionyesha kuwa alitembelea nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na nchini Tanzania ambapo siku za hivi karibuni alikuwa Mkoani Mara Tarime.
Sister huyo amekuwa akitumia mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa pindi anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia vigumu jeshi hilo kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia humu nchini.

0 comments:

Post a Comment