Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Friday, May 3, 2013

Mario Balotelli atoswa na demu wake


MARIO Balotelli ameachwa na aliyekuwa mchumba Fanny Neguesha — siku chache baada ya kuripotiwa kusema kwamba kikosi kizima cha Real Madrid kingeweza kulala nae ikiwa wangeitoa Borussia Dortmund.
Mwanamitindo Fanny, 22, aliondoka kwenye nyumba ya mshambuliaji huyo huko Italia baada ya kugombana kutokana kutoelewana baina ya wawili hao.

Straika huyo wa AC Milan Balotelli, 22, alisema wachezaji wote wa Madrid — akiwemo Cristiano Ronaldo — wangeweza kufanya mapenzi na demu wake Fanny ikiwa juzi wangeweza kufanya maajabu ya kugeuza matokeo ya mechi ya kwanza (4-1) na kufanikiwa kwenda Wembley.

Balo alikaririwa na gazeti la Marca akisema: “Ikiwa Real Madrid wataenda kucheza fainali ya  Champions League, nitamtoa mchumba wangu alale nao wote." Ingawa baadae alikana kutoa kauli hiyo.

Balotelli  aliachana na mama wa mtoto wake wa kike mtangazaji wa TV  Raffaella Fico, 25, kisha ndio akaanzisha mahusiano na mwanamitindo Fanny ambaye ana asili ya Ubelgiji.

0 comments:

Post a Comment