Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Friday, May 31, 2013

Siri ya kuteswa kwa Absalom Kibanda yafichuliwa,sona hapa full story.

Timu ya kuchunguza tukio la kutekwa na
kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa
la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom
Kibanda (pichani), imebaini kuwa kazi
yake ya uandishi wa habari na siasa
vimechangia kuvamiwa kwake na kuna
kutupiana mpira kati ya vyombo vya
dola na vyama vya siasa. Aidha,
uchunguzi wa timu hiyo umebainisha
kuwa baadhi ya watu waliohojiwa
walidai kuwa utekaji wa Kibanda
ulifanywa na vyombo vya dola ukiwa
sehemu ya mpango mkakati wa vyombo
hivyo kukihusisha Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na
vitendo vya ugaidi.
Taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa
tukio hilo ilitolewa jana na Mwenyekiti
wa timu hiyo, Deodatus Balile,
iliyoundwa na TEF katika mkutano wa
pili wa mwaka wa mashauriano kati ya
Baraza la Habari Tanzania (MCT) na
jukwaa hilo jijini Tanga.
“Uchambuzi uliofanywa na timu hii
umebaini kuwa hoja nne zinazungumzwa
kuhusiana na kutekwa na kuumizwa
kwa Kibanda. Hoja hizi ni:- Kazi yake ya
uandishi wa habari, Uhusiano wa kisiasa
na vyama au wanasiasa mbalimbali,
uhusiano wa kijamii ikiwamo mapenzi
na vitendo vya rushwa,” ilieleza taarifa
hiyo.
Alisema timu hiyo imejiridhisha
kutokana na majibu ya wengi kuwa
dhana ya mapenzi na rushwa, havina
nafasi yoyote katika tukio hilo kwani
waliohojiwa walieleza pasi na shaka
kwamba kushambuliwa na kuumizwa
Kibanda halina uhusiano wowote na
rushwa au mapenzi.
Imeeleza kuwa kazi yake ya uandishi wa
habari na siasa vikiunganishwa
vimechangia kuvamiwa kwa Kibanda na
kuna kutupiana mpira kati ya vyombo
vya dola na vyama vya siasa.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa waliohojiwa
waliyataja matukio ya uchaguzi Mdogo
wa Igunga, maandamano ya Morogoro
ya Chadema na mkanda anaodaiwa
kurekodiwa Mkurugenzi wa Usalama wa
Chadema, Wilfred Lwakatare, kuwa
vililenga kukifanya chama hicho
kichukiwe na Watanzania kwa kukitaja
kama chama cha kigaidi ambacho
kinateka watu na kuwaumiza.
“Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe anadai kwamba mpango kama
huo vyombo vya dola viliutumia kwa
NCCR Mageuzi vikakisambaratisha,
Chama cha Wananchi (CUF) kilisingiziwa
udini kikapoteza mwelekeo na sasa
vyombo hivyo vililenga kukifanya
Chadema kionekane cha kigaidi mbele ya
macho ya jamii, ndiyo maana
imerekodiwa mikanda kwa nia ya
kuitumia kujenga hoja hiyo,” taarifa
hiyo ilieleza.
Aidha, baadhi ya watu waliohojiwa
walidai kuwa Chadema kimepewa
mafunzo na ushauri kutoka nje ya nchi
kuwa kikitumia baadhi ya watumishi wa
vyombo vya dola wasiokuwa waaminifu
kuteka, kuumiza na hata kuua baadhi ya
watu maarufu nchini wakiwamo
waandishi na wanasiasa, hivyo
wananchi wataamini kuwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na serikali yake
kimeshindwa uongozi na sasa kimeanza
kazi ya kuua wanaowapinga.
Imeeleza kuwa kwa njia hiyo, hesabu za
Chadema ni kuwa wananchi wataichukia
CCM na Serikali yake na kukipa nafasi
ya kuingia madarakani na kauli ya
Chadema kuwa nchi haitatawalika
itakuwa imetimia.
Taarifa zaidi ya kamati hiyo imebainisha
kuwa maisha ya wanahabari yapo
hatarini kutokana na makundi mengi
yenye maslahi kuwaona wanahabari
wanaosimamia ukweli kuwa maadui wa
maslahi yao haramu.
“Kuna hatari kubwa inayowakabili
waandishi wakati nchi inapoelekea
kwenye uchaguzi wa mwaka 2015,”
taarifa hiyo ilisema.

    Source-nipashe

K Lynn afichua siri,kumbe mapacha wake wawili ni watoto wa Mengi.Cheki pic hapa...

Hatimaye miss Tanzania mwaka 2000 amefichua baba halisi wa watoto wake mapacha.Cheki alichokisema hapa...

Thursday, May 30, 2013

Ombaomba feki akamatwa mjini Iringa,soma story nzima hapa...

WAKAZI wa mjini Iringa hivi karibuni
wameshuhudia kituko cha mwaka baada ya
kumnasa mzee mmoja akijifanya ombaomba
kwa kuigiza ulemavu asiokuwa nao.
Ombaomba huyo feki alijifanya hana mkono
wa kushoto na mguu wa kulia na kuweka pozi
la kuomba kama vile ni mlemavu katika eneo
la Hazina Ndogo, mjini hapa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,
mlemavu huyo feki ameumbuliwa na mtu
mmoja ambaye alimuona asubuhi ya siku ya
tukio akiwa hana ulemavu wowote kabla ya
kumkuta mchana akiomba kwa kujifanya ni
mlemavu wa mkono na mguu.
Mtu huyo aliwaambia baadhi ya wananchi siri
ya ombaomba huyo na kuwafanya kupandwa
na hasira na kuanza kumshushia kipigo
wakitaka kuhakikisha kama kweli ni mzima
kiasi cha kumuumiza usoni.
Kwa hofu ya kuuawa, mlemavu huyo feki
alijinusuru kwa kuonesha mkono wake wa
kushoto aliokuwa ameuficha ndani ya koti
alilolivaa na mguu aliokuwa ameukunja na
kuukalia.
Wakati wananchi wenye hasira wakiendelea
kumpiga, mzee huyo alijitahidi kupata upenyo
na kutimua mbio ndefu kukimbilia eneo la
Miyomboni na kuwaacha watu wengine wakiwa
hawana mbavu kwa vicheko.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
walipoongea na mwandishi wetu walisema
wakati mwingine ombaomba huyo hujifanya
bubu na kuwaomba watu fedha za matibabu.
Inadaiwa kuwa hii si mara ya kwanza kwa
ombaomba huyo kushtukiwa akifanya mchezo
huo, awali alishawahi kufukuzwa katika
Kitongoji cha Santoni mjini hapa.
“Bahati yake amekimbia kama tukimkuta tena
akijidai ni mlemavu tutamvunja mkono na
mguu ili awe mlemavu kweli,” alisema mmoja
wa mashuhuda wa tukio hilo.
Tuhuma nyingine zinasema kuwa ombaomba
huyo hutumia mbinu hizo za kitapeli kwa
kuwa amekimbiwa na mpenzi kutokana na
kutokuwa na kipato.
Wananchi hao wenye hasira wameutaka
uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana
ombaomba wote wanatumia udanganyifu
kujipatia fedha na kutaka kuwepo kwa
utaratibu maalum wa kuwasaidia wanaohitaji
misaada ya kweli.

Tuesday, May 28, 2013

R.I.P Mangwear,Soma hapa chanzo cha kifo chake...


Taarifa Kutoka South
Africa Kutoka Kwa Hussein
Original Ambaye Yupo Pretoria
Amesema Ngwear Amefariki Leo
Asubuhi. Alikuwa Ghetto Moja Na
Msanii M To The P.
Walivyokwenda Kuwagongea
Asubuhi Walikuta Ngwear
Amefariki Na M To The P
Amepoteza Fahamu Kabisa. Pia
Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa
Watu Wa Karibu Wa Ngwear
Huko South Africa. Ngwea akiwa na msanii M
to the P jana south africa.mtu wa karibu
anasema walitakiwa kurudi dar leo lakini
waliwakuta wamezima kwenye room wote
wawili baada ya kuji overdose madawa ya
kulevya na M to the P yupo hoi hospitali.

Friday, May 24, 2013

Wahu na Nameless watarajia kupata mtoto wa pili


Couple ya mastaa kutoka Kenya, Wahu na Nameless inategemea kuungana na couples za mastaa wengine duniani kama Kim Kardashian na Kanye West, kupokea ujio wa member mpya katika familia zao kutokana na Wahu kuwa mjamzito wa mtoto wa pili.
wahunameless-2
Baada ya kuwepo uvumi kuwa Wahu ni mjauzito wa mtoto wao wa pili, hitmaker huyo wa ‘Sweet love’ amethibitisha kuwa kweli na anategemea kujifungua mapema mwezi August mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa facebook Wahu alimjibu fan mmoja ambaye ni miongoni mwa fans wengi waliokuwa wakitaka ukweli kuhusu uvumi huo ambao ulithibitishwa kwa jibu lake fupi, “Yes I am”.
Akiwa na excitement ya mtoto wa pili Wahu pia anategemea kuachia single mpya mwishoni mwa wiki hii, wimbo ambao Wahu aliuambia mtandao wa standard media wa Kenya kuwa itakuwa ni hit song kama ilivyokuwa “Sweet Love” na “Running Low”.
Mtoto wa kwanza wa Nameless na Wahu aitwaye Tumiso Nyakwea alizaliwa mwaka 2006 na wimbo wa “Sweet Love” ulikuwa ni dedication kutoka kwa mama yake, na ni wimbo ambao umemletea matunda ya tuzo kadhaa.
Wanamuziki na wanandoa hao, walifunga ndoa 2005, ambayo imefanikiwa kutoa majibu ya mtoto wa kike anayetegemea kupata mdogo wake soon.                                                                                                                 Source;Bongo  5

Picha za mwanasheria aliyebambwa akifanya ukahaba. Ashitaki mawakili kwa kusambaza picha zake za uchi

Mwanasheria mmoja wa Illinois ambaye alipatikana na hatia ya kufanya ngono na mwanaume mmoja kwa malipo ya Dola za Marekani 100 anamshitaki aliyekuwa wakili wake wa utetezi na mawakili wengine wawili kwa madai ya kusambaza picha zake za utupu.

Reema Bajaj, mwenye miaka 27, anasema wakili wake wa zamani Timothy Johnson, mwendesha mashitaka wa zamani Calvin Campbell, na mwanasheria aliyeorodheshwa kwenye hati ya mashitaka kama ‘John Doe’ walitoa hadharani picha zake za siri sambamba na taarifa kumhusu yeye.






DR SLAA NA MPENZI WAKE RUKSA KUOANA!



HATIMAYE Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi( KWA SASA NI MCHUMBA WA DR. SLAA) , Maimbo baada ya kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria.

Hukumu hiyo ya rufaa ya madai ya ndoa Na.32/2012 ilitolewa leo na Hakimu Aniseth Wambura ambapo alisema mahakama yake imefikia uamuzi huo wa kuitupa rufaa hiyo kwasababu haina mantiki ya kisheria.

Hakimu Wambura alisema mahakama yake imekubalina na hukumu iliyotolewa Aprili 2012 na Mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya madai talaka iliyokuwa imefunguliwa na Mushumbusi anayetetewa na wakili wa kujitegemea Philemon Mutakyamilwa dhidi ya Maimbo ambapo mahakama hiyo ya chini ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao kwasababu Maimbo alikuwa ni mzinzi, simwaminifu katika ndoa yake na alikuwa akimtesa mkewe.

“Baada ya mahakama yangu kusikiliza hoja za mwomba rufaa na mjibu rufaa ,mahakama hii imefikia uamuzi wa kukubali hoja za Mushumbisi kuwa kwa tabia ile ya mbaya ya uzinzi na ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake hapakuwepo na ndoa baina yao hivyo mahakama yake inatangaza kuwa hukumu ya mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo iliivunja ndoa hiyo ilikuwa hukumu sahihi “alisema hakimu Wambura.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili Mutakyamilwa alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwani mahakama imetenda haki kwasababu kesi hiyo ya madai ya talaka ilikuwa na msukumo wa siasa chafu zilizokuwa na lengo chafu la kumchafulia jina mteja wake(Mshumbusi) ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzie Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa.

Thursday, May 23, 2013

Kiingereza cha Diamond chazua balaa Instagram,fans wake wamuumbua kwa kiingereza kibovu

NANUKUU..!! "after I done did the Uk, Congo, Burundi... GUESS Where next I'll be headed??????????????!!!!!!!!!!!.........""" mwisho wa kunukuu 
teh teh teh!!
 
credits;Zeddylicious Blog

Wednesday, May 22, 2013

Cheki baadhi tu ya picha ya jinsi hali ilivyokuwa leo Mtwara masaa machache yaliyopita



Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu. Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo. Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo. 
Kituo kimoja cha habari kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao) 
Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar. 
Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe. 
Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali. 
Maeneo yote yametawaliwa na ukimya

Paul Okoye wa P’Square akana mtoto wa pili aliyezaliwa na msichana mwingine siku 3 kabla ya girlfriend wake Anita kujifungua


Habari za kutatanisha zinazomhusu Peter Okoye wa kundi la muziki lenye mafanikio makubwa kutoka Nigeria P’Square zinasema kuwa msichana mmoja aitwaye Elshama Benson Igbanoi ambaye ni mpenzi wa siri wa Paul amejifungua mtoto wa kiume na kudai kuwa ni wa staa huyo.
pp
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Nigeria, Elshama mwenye miaka 19 alijifungua mtoto huyo wa kiume April 7, 2013 huko London Uingereza wakati girlfriend wa sasa wa Paul aitwaye Anita alijifungua mtoto wa Paul April 10, 2013 huko Atlanta Marekani, hivyo kumfanya mtoto wa Anita awe ni wa pili kwa Paul na si wa kwanza kama ilivyokuwa ikifahamika awali.
Chanzo kimesema Elshama aliyewahi kuwa miss alijifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya Queen Charlotte and Chelsea Hospital iliyoko London Uingereza na kisha aliwasiliana na baba wa mtoto wake ambaye ni Paul ambaye hata hivyo alimkana mtoto na kumwambia ana mpango wa kwenda London kwaajili ya kufanya vipimo vya DNA kuthibitisha kama kweli mtoto huyo ana damu yake.
paul n elshama
Elishama alisema hajawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine na amekuwa mwaminifu kwa Paul toka alipomtoa bikra akiwa na miaka 17.

Rais Obama kutua Tanzania Julai Mosi


Wakati Ikulu ya Marekani ikitangaza kuwa Rais Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu kuanzia Julai Mosi hadi 3, Serikali ya Tanzania imesema ujio huo utasaidia kuinua uchumi kutokana na kufaidika na uwekezaji na misaada mbalimbali. 
Rais Obama anatarajiwa kuzitembelea Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Taarifa ya Ikulu ya Marekani iliyotolewa na Ubalozi wa nchi hiyo nchini, inasema Rais Obama atazuru Afrika kuanzia Juni 26 hadi Julai 3, ikiwa ni moja ya sehemu ya kuimarika uhusiano baina ya nchi yake na bara la Afrika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma alisema ziara ya kiongozi huyo inatarajiwa kuinufaisha Tanzania maeneo ya biashara na uchumi.
Rais Obama ambaye ana asili ya Kenya ambako anatoka baba yake mzazi, baada ya kuchaguliwa kushika madaraka nchini mwaka 2009, alimwalika Rais Kikwete akiwa kiongozi wa kwanza kwenda Marekani kujadiliana masuala mbalimbali.
Ziara yake ya kwanza kwa bara la Afrika aliifanya nchini Ghana ambako alihutubia Bunge.

Mr nice azomewa na mashabiki nchini Kenya



Mtandao wa ghafla kutoka Kenya umeripoti kuwa, msanii Mr Nice, amejikuta akizomewa na umati wa watu waliokuwa katika Club moja inayoitwa I club, ambapo wachekeshaji Fred Omondi na Mc Antonio hufanya show zao pale kila siku za jumapili.

Inasemekana Mr Nice alikua ameenda pale kwa ajili ya kula good time tu, na kufurahisha nafsi yake, lakini matokeo yake hayakuwa kama alivyotarajia....

Aibu ilianza pale mchekeshaji Mc Antonio alipomuona Mr Nice katikati ya watu, na kwakuwa ni mtu maarufu, Mc akamuambia awapungie mikono watu waliokuwepo pale...

Mr Nice hakufanya hivyo wala kusimama akidai kuwa yeye ni msanii ambae amesainiwa na mtu mwingine na Mc huyo hawezi kumlipa yeye, na akipanda jukwaani hapo atashitakiwa na magement yake.

" Hamnilipi ninyi... nikipanda hapa kwenye jukwaa, nitashtakiwa mimi"..Mr.Nice

Baada ya kusema maneno hayo mashabiki walianza kumzomea huku wakipiga kelele wakisema Mac "Muga" wimbo wa Ally Kiba, ambao unasemekana kuwa unamdiss yeye. na dj hakuwa na hiyana aliupiga wimbo huo maana mashabiki waliutaka.

Tuesday, May 21, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YABAINIKA NI UOZO MTUPU".....SIFURI KIBAO ZAFUTWA KIMYA KIMYA

MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu kwa wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo ya mitihani yao yanaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa kuzua aibu na kama si uamuzi uliotajwa bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu za zamani, matokeo hayo yangeibua aibu kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne, 2012.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa kutosha. 

“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya na si za zamani. Vyuo vikuu nchini visingeweza kupata wanafunzi wa kutosha.

"Tatizo hapa si uwezo wa wanafunzi moja kwa moja katika kumudu mitihani bali ni kufanywa kwa mabadiliko ya alama bila kuwaandaa.

" Alama hizi zilipaswa kuanza kutumika na wanafunzi wapya, yaani kama wanaanza kidato cha kwanza wawe wanapewa mitihani ya kupimwa kwa kuzingatia alama mpya na waendelee nazo hadi mitihano yao ya mwisho. 

“Na hivyo hivyo kwa wanafunzi wa kidato cha sita. Alama hizi mpya zinapaswa kutumika kwako kuanzia wakiwa kidato cha tano mara wanapoanza shule, kila mitihani wanayopewa isahihishwe na kupangiwa alama kwa kutumia hizi alama mpya,” kinaeleza chanzo chetu cha habari kutoka NECTA. 

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo ya alama, alama mpya zilizokuwa zimetumika awali ni daraja F kuanzia 34 hadi sifuri; badala ya alama hiyo F kuanzia 20 hadi 0; daraja D kwa kuzingatia alama mpya linapaswa kuanzia 35 tofauti na awali, yaani alama 21. 

Taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, kati ya sababu za kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita tofauti na muda uliotarajiwa yaani mwanzoni mwa Mei, ni pamoja na upangaji upya matokeo hayo, ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa kwa kidato cha nne ambapo matokeo yalitangazwa na kisha kufutwa ili kuyapanga upya kwa kutumia alama za zamani. 

Lakini alipoulizwa kuhusu masuala hayo ndani ya NECTA, Ofisa Habari wa Taasisi hiyo nyeti nchini, John Nchimbi alisema; “Kwa sasa niseme tu kwamba mchakato wa kuandaa matokeo ya kidato cha sita unaendelea, siwezi kusema lini hasa utakamilika lakini nina uhakika ni katika muda muafaka.” 

Kuhusu matokeo ya kidato cha sita kucheleweshwa kutokana kupangwa upya ili kupunguza idadi ya waliofeli kutokana na matumizi ya alama mpya za kufaulu, Nchimbi anasema; “Unajua haya maagizo haya ya bungeni (kupanga matokeo kwa kuzingatia alama za zamani) yamekuja wakati mchakato wa kuandaa matokeo ulikwishaanza. Kwa hiyo baada ya maagizo ilibidi kufanya kazi hiyo tena kwa kufuata maagizo hayo.” 

Hata hivyo, hakuweka bayana kama matokeo ya awali kabla ya maagizo ya Serikali yaliyotolewa bungeni kutumia alama za zamani yamewafanya wanafunzi wengi kufeli na badala yake akasema; “Hilo siwezi kulizungumzia kwa sababu mchakato wa matokeo hayo haukuwa umefika mwisho. Takwimu rasmi hazikuwa zimekamilishwa. Kwa hiyo si sahihi kusema rasmi walifeli.” 

Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa matokeo yanayotarajiwa ya kidato cha sita, taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, baada agizo la serikali la kufuta na kurejewa upya kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012, takriban wanafunzi 50,000 wamepata unafuu katika matokeo yao tofauti na awali. 

Awali, kwa kuzingatia matokeo ya kidato cha nne mwaka jana yaliyotangazwa Februari, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa, jumla ya watahiniwa 126,847 tu kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya mtihani huo walifaulu. 

Katika matokeo hayo idadi ya wasichana waliofaulu ilitajwa kuwa ni 46,181 wakati wavulana waliofaulu ikiwa wanafunzi 80,686 na idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 16,112 kati yao watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani wasichana ni 6,7751 na wavulana 9,361. 

Katika matokeo hayo watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, daraja la pili 6,453 na daraja la tatu ni 15,426, wakati waliopata sifuri ni 240,903 lakini kwa kuzingatia taarifa za vyanzo vyetu ndani ya Baraza, idadi hiyo itabadilika kwa sababu ya alama kuongezwa kwa watahiniwa hao wa mwaka 2012. 

Lakini matokeo hayo yalitangazwa pamoja na vituko walivyofanya baadhi ya wanafunzi, vikiwamo vituko vya kuandika matusi kwenye karatasi za majibu ya mitihani na kutokana na makosa hayo, watahiniwa 789 walifutiwa mitihiani yao. 


                    Source;raia mwema

BAADA YA TID KUTEMWA TUZO ZA KTMA, SASA KAPATA SHOW NCHINI UINGEREZA SIKU YA FAINALI ZA KTMA.

TID hatokuwa na usiku mbaya June 8 wakati tuzo za Kili zitakapokuwa zikitolewa kwakuwa atakuwa mbali akipiga show ya kimataifa na hitmaker wa Kigeugeu, Jaguar wa nchini Kenya.
581935_10151686509932642_886089228_n
Hivi karibuni TID aliwalalamikia waandaji wa tuzo za Kili kwa kutoujumuisha wimbo wake kwenye tuzo za mwaka huu. Pia wiki iliyopita, alitangaza kujitoa kwenye list ya wasanii watakaomsindikiza Lady Jaydee kwenye show yake ya May 31.

chanzo : bongo 5

Saturday, May 18, 2013

NISHA AMKIMBIZA WEMA KWA KUMILIKI NYUMBA YA KIFAHARI, HII NDO NYUMBA YA NISHA YENYE THAMANI YA MILIONI 95. ICHEKI HAPA


Stori:Gladness Mallya
Unakumbuka zile habari za Wema Isaac Sepetu kununuliwa jumba la kifahari na bilionea mmoja Kijitonyama, Dar? Sasa zimegeukia kwa staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye naye kuna madai mazito ya kuhongwa nyumba.

Ilikuwa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo gazeti hili lilipokea ujumbe mfupi wa simu ya mkononi ‘sms’ kutoka kwa chanzo chake.
HABARI ILIVYOANZA
Chanzo: Hivi ninyi mna habari?
Risasi Jumamosi: Nyingi tu lakini kama una ya kwako itatufaa sana.
Chanzo: Kwa taarifa yenu Nisha kanunuliwa bonge la mjengo hapa Kijitonyama karibu kabisa na Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’.
Risasi Jumamosi: Nani kamnunulia?
Chanzo: Nasikia ni bilionea mmoja mwenye fedha zake hapa Dar es Salaam, kainunua kisha kamhonga Nisha kwa sababu ni mpenzi wake.
Risasi Jumamosi: Tunashukuru kwa taarifa, kaa mkao wa kula itaruka hewani mara moja baada ya upelelezi wetu.
RISASI LATUA KIJITONYAMA
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilisaga soli hadi maeneo hayo na kuanza kugonga geti moja baada ya lingine hadi lilipofanikiwa kuinasa nyumba hiyo huku Nisha akiwa ndani kapumzika.
Msichana aliyejitambulisha kuwa ni dada wa kazi au hausigeli kwa lugha laini ndiye aliyetoboa siri kuwa ni kweli staa huyo yupo ndani na amehamia mahali hapo muda si mrefu.
RISASI LAINGIA MJENGONI
Risasi Jumamosi liliomba kukaribishwa ndani ili kupata ‘ditelzi’ na ndipo Nisha akaamka na kuamua kuacha paparazi wetu apige picha japo awali alitia ngumu akidai hayuko tayari kuianika nyumba hiyo.
Ndani ya nyumba hiyo yenye vyumba vitano, sebule, jiko, choo na mabafu mawili, anayeishi Nisha na dada wake wa kazi, kuna samani nyingi za bei mbaya, mazagazaga kibao, mazulia na marumaru huku kila kona kukiwa na Tv ya flat screen hadi chooni (angalia picha Uk.1).
NISHA ABANWA KUHUSU UMILIKI
Nisha anayemiliki kampuni ya kuzalisha muvi za Kibongo ya Nisha’s Film Production alipotakiwa kueleza kama kanunua, kanunuliwa au kapangisha nyumba hiyo, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni juhudi zangu binafsi jamani, kujituma sana kwenye kazi yangu ya filamu. Kuhusu kununua au kupangisha naomba nikimaliza ‘process’ f’lanif’lani ndipo nitaweka wazi, kwa sasa bado ni mapema mno.”
Risasi Jumamosi: Kuna madai kuwa umehongwa hii nyumba na bilionea mmoja wa hapa Dar, je, ni kweli?
Nisha: Hakuna kitu kama hicho jamani, hayo ni maneno ya watu wasiojituma kufanya kazi kwa bidii. Haya ni matunda ya kufanya kazi sana.
Risasi Jumamosi: Nyumba hii ina samani mpya zote za thamani kubwa sana, je, zimegharimu fedha kiasi gani?
Nisha: Vitu vyote vya ndani hadi nikahamia vimegharimu karibu Sh. milioni 95. Ni fedha zilizotokana na mauzo ya filamu zangu nne nilizotengeneza mwenyewe mwaka jana.
Risasi Jumamosi: Kuna madai kuwa umejiunga Freemason ndiyo maana ndani ya kipindi kifupi mambo yako safi, je, ni kweli?
Nisha: Nimesikia hizo tetesi za Freemason ‘but’ naamini mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe. Mimi namwachia Mungu, namuomba kila siku anipe baraka zake, namshukuru na nazidi kumuomba nifanikiwe.TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Baada ya Mbunge wa chadema kuzushiwa kwenye scandal ya kufanya mapenzi ya jinsia moja,haya ndo maneno aliyojibu mbunge huyo.


Kupitia season mpya ya Clouds Fm, ndani ya so so fresh na fetty, Mh Halima Mdee jana amefunguka juu ya swali aliloulizwa kuhusu story zilizosambaa kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja.
aah unajua huwezi kuzuia watu kusema, na mimi huwa sihangaiki na watu wanasema nini, lakini ukitaka kumjua Halima unaweza ukamchunguza kirahisi sana, kwa kumuangalia alipotoka, historia yake na mahusiano yake, ambayo mengine ni wazi sana watu walikuwa wanayajua, 
watu wanapenda ku speculate pale ambapo wanaona kitu ambacho hawati  kuona, sasa hilo swala lilishaandikwa sana, nadhani walioandika baadae wakaja kuomba radhi kwasababu waligundua wameandika kitu kisicho sahihi, probably kutokana na sauti yangu you know, probably kutokana na tembea yangu, kwasababu mimi nimekulia kwenye familia ya wanaume watupu umeona eeh, mimi nimekuwa ni mpambanaji tokea utotoni, kwasababu nimezungukwa na jeshi la kibabe, thats who iam, lakini mtu anaetaka kumjua Halima na ana uhuru tu, hata akitaka niwatajie list ya watu wangu i can do that, lakini sidhani kama is their damn business, cause ma life is personal, na wakitaka kuchunguza wachunguze kwa mpango wao na watapata taarifa, kwa uhuru tu, na wanaweza wakatoa tangazo kwamba jamani watu waliowahi kuwa na uhusiano na huyu if any wajitokeze, watajitokeza kama wapo upande huo, watajitokeza kwasababu sasa hivi si dunia huru bana ......

HII NDO LIST YA WATU MAARUFU KUTOKA KENYA NA TANZANIA, AMBAO WAMETAJWA NA MTANDAO WA KENYA KUA NI MAFREEMASON. DIAMOND NAE KATAJWA


Inawezekana kila kitu kina wakati wake, kuna muda watu walikuwa wakisikia neno ‘Freemason’ ama ‘Illuminate’ kama inavyojulikana nchini Kenya wengi walikuwa wanaiona ni habari kubwa, lakini kwa sasa hivi inaweza kuchukuliwa kama sio big deal.

Sababu ni ile ile kuwa wengi wanaoendelea kwa haraka ama kuwa juu katika kile wanachokifanya basi utasikia huyo ni member wa Freemason, kwa upande wa Marekani wanasema ‘he/she just sold her/his soul to the devil’.  Japo kwa upande wa Marekani wapo wanaokiri kufanya hivyo kweli, ila kwa Africa Mashariki hakuna msanii aliyewahi kukiri.
Lakini yote hayo ni kama yanakanganya na kuonekana kama hayana mantiki hasa pale ambapo vithibitisho vya kinachoongelewa huwa havileti mantiki ya moja kwa moja. Pengine watu wanatafuta pesa kwa bidii na kumuomba Mungu lakini kwa kuwa kwenye mstari wa juu wanajikuta wanahisiwa kuwa member wa secret society (Freemason). Oh..au labda ndo vile kwa upande mwingine lisemalo lipo na kama halipo laja !
Tunathubutu kuziita blaa blaa kwa upande mwingine, lakini tukiweka kwenye mabano kuwa inaweza kuwa na ukweli, who knows!
Mtandao wa malimwengu wa nchini Kenya huenda ukawa na mfano mzuri wa kile nilichokitaja hapo juu, mtandao huo kupitia mwandishi wake imetaja majina ya wasanii wa Tanzania na Kenya wanaosemekana kuwa ni wafuasi wa Freemason, lakini kizuri zaidi ni kwamba mtandao huo umejaribu kuonesha vithibitisho na kushindwa kupata jibu la moja kwa moja kwa nini wasanii hawa wamekumbwa na hili. Inabaki hivyo hivyo kuwa tetesi tu.
Hawa ni wasanii waliotajwa na maelezo yanayowahusu:
TANZANIA:
1.Naseeb Abdul Jumaa (Diamond Platinum)
Picha aliyopiga mwaka jana akiwa na mzungu anaeaminika kuwa ni moja kati ya viongozi wa Freemason wakiwa wameweka pozi na kuonesha ishara inayooaminika kuwa ni ya Freemason, na kwamba alipoulizwa yeye alisema hakufahamu kama alikuwa anaelekezwa kupiga picha kwa pozi la ki-freemason. Kwa mujibu wa mwandishi anaona inaweza kuwa kweli kwa sababu anaonekana kuenjoy!
2.Ali Kiba
Iliwahi kusemekana pia kuwa Ali Kiba ni Freemason, na wewe pia unaweza kufikiria sababu kwamba eti alikuwa maarufu sana na baadae kufifia. Maoni ya mwandishi (Hakuna uthibithibisho/ushaidi unaoweza kuwekwa thidi yake).
   
3.Jacquelin Wolper

Ni muigizaji maarufu wa kike mtanzania. Maoni ya mwandishi ( Hakuna ushaidi, tetesi peke yake hazina umuhimu)
KENYA:
1.Camp Mulla
Maoni ya mwandishi (Hapana, sio kweli. Sababu ya kufanikiwa kwenye muziki haimaanishi kuwa ni members wa Freemason. Hakuna mtu mwenye ushahidi kuwa Camp Mulla ni members wa Freemason).
2.Octopizzo
Maelezo yanayomhusu yanaonekana kuwa mengi sana kama kawaida, ni moja kati ya wasanii ambao tetesi za kuwa illuminate ni nyingi zaidi.
3.Nonini
Ukimtaja Nonini kama Illuminati lazima kitu serious zaidi kiandikwe ama ikielezwe. Nonini sio Illuminati (maoni ya mwandishi).
Hao ndio waliandikwa na kutolewa maoni ama maelezo na muandishi wa mtandao huo. Lakini tetesi huwa nyingi na kuongezeka mara kwa mara kwani hata Avril pia huwa anatajwa kuwa Illuminati na kwamba kazi yake ni kueneza usagaji nchini humo na eti sababu mojawapo ni mashairi ya wimbo wake ‘Chokoza’.
Haya yote yanasemwa tu, cha kufanya ni kile alichokisema Prof. Jay kwenye wimbo wake ‘Bongo Dar es Salaam’...  “Akili kumkichwa, ukizubaa unaachwa feli”.

KUA WA KWANZA KUMCHEKI MTU HUYU WA AJABU : ANAMENYA NAZI 500 KWA MDOMO....AINGIA KWENYE KITABU CHA GUINESS


A man in Panama with indestructible teeth, astonishing jaws of steel and anawesome resemblance to Mr. T is gnawing his way toward a Guinness World Record.

At 64-years-old, Andres Gardin -- who chomps under the moniker "Coconut Peeler" -- is vying for immortality in the Guinness Book of World Records, with his ability to shuck 500 coconuts in six hours. He proved the feat last September, MSN reports.
He's been honing his peeling skills since he was 11 and says he has shredded more than 100,000 coconuts in his lifetime, AFP reports.
The master of the hairy fruit recently proved his skills on a disheveled basketball court in Panama after he peeled off a coconut's hardened skin in an impressive eight seconds.
"Peeling coconuts is not as easy as you all think," Gardin told a group of fans. "To peel coconuts, you've got to have jaw power. You've got to have teeth power," AFP reported.
While Guinness officials have yet to verify Gardin's record, he is determined to get world-reconigition for his feats of strength.
"I want to get in the Guinness Book, because I know that I have what it takes," he said.
His oral skills don't stop there. On May 10, Gardin, who drives a cab as his day-job, demonstrated his impressive dental strength to a crowd of onlookers in Rio Alejandro, about 85 km north of Panama City, when he dragged two cars by his teeth through a crowd of flabbergasted onlookers.
credits-BongoClantz

MAPITIO YA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 18 MEI 2013


DSC 0262 5766dDSC 0263 ef14a
DSC 0264 e160a

DSC 0265 784f3
DSC 0266 58f60
DSC 0267 c101d
DSC 0268 5e9e8
DSC 0269 f7c59
DSC 0270 80e8c 
 DSC 0271 21f95