Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Friday, May 31, 2013

Siri ya kuteswa kwa Absalom Kibanda yafichuliwa,sona hapa full story.

Timu ya kuchunguza tukio la kutekwa na
kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa
la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom
Kibanda (pichani), imebaini kuwa kazi
yake ya uandishi wa habari na siasa
vimechangia kuvamiwa kwake na kuna
kutupiana mpira kati ya vyombo vya
dola na vyama vya siasa. Aidha,
uchunguzi wa timu hiyo umebainisha
kuwa baadhi ya watu waliohojiwa
walidai kuwa utekaji wa Kibanda
ulifanywa na vyombo vya dola ukiwa
sehemu ya mpango mkakati wa vyombo
hivyo kukihusisha Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na
vitendo vya ugaidi.
Taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa
tukio hilo ilitolewa jana na Mwenyekiti
wa timu hiyo, Deodatus Balile,
iliyoundwa na TEF katika mkutano wa
pili wa mwaka wa mashauriano kati ya
Baraza la Habari Tanzania (MCT) na
jukwaa hilo jijini Tanga.
“Uchambuzi uliofanywa na timu hii
umebaini kuwa hoja nne zinazungumzwa
kuhusiana na kutekwa na kuumizwa
kwa Kibanda. Hoja hizi ni:- Kazi yake ya
uandishi wa habari, Uhusiano wa kisiasa
na vyama au wanasiasa mbalimbali,
uhusiano wa kijamii ikiwamo mapenzi
na vitendo vya rushwa,” ilieleza taarifa
hiyo.
Alisema timu hiyo imejiridhisha
kutokana na majibu ya wengi kuwa
dhana ya mapenzi na rushwa, havina
nafasi yoyote katika tukio hilo kwani
waliohojiwa walieleza pasi na shaka
kwamba kushambuliwa na kuumizwa
Kibanda halina uhusiano wowote na
rushwa au mapenzi.
Imeeleza kuwa kazi yake ya uandishi wa
habari na siasa vikiunganishwa
vimechangia kuvamiwa kwa Kibanda na
kuna kutupiana mpira kati ya vyombo
vya dola na vyama vya siasa.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa waliohojiwa
waliyataja matukio ya uchaguzi Mdogo
wa Igunga, maandamano ya Morogoro
ya Chadema na mkanda anaodaiwa
kurekodiwa Mkurugenzi wa Usalama wa
Chadema, Wilfred Lwakatare, kuwa
vililenga kukifanya chama hicho
kichukiwe na Watanzania kwa kukitaja
kama chama cha kigaidi ambacho
kinateka watu na kuwaumiza.
“Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe anadai kwamba mpango kama
huo vyombo vya dola viliutumia kwa
NCCR Mageuzi vikakisambaratisha,
Chama cha Wananchi (CUF) kilisingiziwa
udini kikapoteza mwelekeo na sasa
vyombo hivyo vililenga kukifanya
Chadema kionekane cha kigaidi mbele ya
macho ya jamii, ndiyo maana
imerekodiwa mikanda kwa nia ya
kuitumia kujenga hoja hiyo,” taarifa
hiyo ilieleza.
Aidha, baadhi ya watu waliohojiwa
walidai kuwa Chadema kimepewa
mafunzo na ushauri kutoka nje ya nchi
kuwa kikitumia baadhi ya watumishi wa
vyombo vya dola wasiokuwa waaminifu
kuteka, kuumiza na hata kuua baadhi ya
watu maarufu nchini wakiwamo
waandishi na wanasiasa, hivyo
wananchi wataamini kuwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na serikali yake
kimeshindwa uongozi na sasa kimeanza
kazi ya kuua wanaowapinga.
Imeeleza kuwa kwa njia hiyo, hesabu za
Chadema ni kuwa wananchi wataichukia
CCM na Serikali yake na kukipa nafasi
ya kuingia madarakani na kauli ya
Chadema kuwa nchi haitatawalika
itakuwa imetimia.
Taarifa zaidi ya kamati hiyo imebainisha
kuwa maisha ya wanahabari yapo
hatarini kutokana na makundi mengi
yenye maslahi kuwaona wanahabari
wanaosimamia ukweli kuwa maadui wa
maslahi yao haramu.
“Kuna hatari kubwa inayowakabili
waandishi wakati nchi inapoelekea
kwenye uchaguzi wa mwaka 2015,”
taarifa hiyo ilisema.

    Source-nipashe

0 comments:

Post a Comment