Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu,
hatimaye mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
ameamua kujibu shutuma za Lady Jaydee dhidi yake. Ruge amekitumia
kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM, kujibu rasmi shutuma hizo.
Amesema anasikitishwa na jinsi Jaydee anavyoendesha harakati zake na kudai kuwa anapigana kwenye vita isiyo sahihi.
“Jaydee akaze buti, anapigana na
wrong war, vita yake ameidirect tofauti na mizinga yake, bunduki zake
amezielekeza kusiko. Skylight Band inamsumbua, akubaliane na ukweli
kwamba Skylight ndio iliyoisababishia Nyumbani Lounge kushuka
ilivyoshuka, sio Lady Jaydee kama msanii.
Vita yake na bunduki zke azielekezee
Skylight Band.Hajazungumza hata mara moja kwamba ndio kitu
kinachosumbua. Mimi naamini kabisa akifanya hiyo kazi, Jaydee bado ni
msanii mzuri, ana nguvu, afanye kazi kubwa ya kuweza kurudisha mapambano
yake kisanii, kufanya kazi na aangalie tatizo lililotokea Nyumbani
Lounge labda anaweza akatatua matatizo lakini sio kushambulia watu
kwenye mitandao,” amesema Ruge.
Hata hivyo amesema yupo tayari kukaa meza moja na Lady Jaydee kuzungumza na kumaliza tofauti zao.
“Mimi niko tayari, kesho, kesho
kutwa, kama yupo tayari na ana watu wengine wengi tu ambao wanahisi kuna
matatizo binafsi ya kuongea na Clouds, twende sehemu nyingine neutral
tu, tukodishe, tukae pale tusikie matatizo.
Haisaidii muziki wetu kuonekana Bongo
Flava ni watu ambao kutwa ni kulalamika, kutwa ni maneno na matusi tu
pale panapokuwa na matatizo.”
Ameongeza kuwa suala la wasanii wa
Bongo Flava kupenda kutukana limewafanya hata wasambaji wa muziki nchini
kuacha kufanya kazi nao.
“GMC kampuni iliyowapa pesa nyingi
wasanii kwenye biashara sio kuwapa tu kwa kuwagawia, kwa kufanya nao
biashara, sasa hivi huu ni mwaka wao wa pili na nusu hawajatoa hata
albam moja ya Bongo Flava.
Wasanii wa Bongo Flava wanafikiria kwa Mamu pamefungwa lakini Mamu anaendelea na wasanii wa Gospel na wanauza vile vile.
Ruge amewaasa wasanii wa Tanzania
akiwemo Lady Jaydee kuzitumia vizuri fursa za kiuchumi zinazojitokeza na
sio kupenda kulalamika.
“Turudi kwenye mstari wa kuziona
opportunities, turudi kwenye mstari wa kusema kwamba leo tunataka
kumzungumzia Jaydee akiwa na perfume, akiwa na lipstick kama jana
iliyozinduliwa na Rihanna ambayo nikaambiwa kwamba stock ya lipstick
mpya ya Rihanna iliyozinduliwa ilikwisha baada ya masaa matatu.
That’s how bigger brand is supposed
to be, and that’s how powerful a brand is supposed to be katika namna ya
kuunganisha na fursa zilizopo. Unapokuwa na jina tumia fursa, tumia
opportunities zinazokuijia wewe kujiendeleza na kujikuza.
Lakini suala la kulaumiana
halitatukuza kwasababu sisi ni radio binafsi, tutafanya kile
tunachokifanya sisi kwa matakwa ya wasikilizaji wetu wengi zaidi,
tukiiangalia faida kama motivation, tukiiangalia social responsibility
kama motivation yetu ya pili, in the long run kuangalia tunakotaka
kwenda kufikia strategy ambayo kampuni yetu inajiwekea.”
Ruge pia amewakumbusha wasanii kutojisahau kwakuwa hakuna msanii anayeweza kuhit maisha yake yote.
“Tuwaandae wasijisahau, na katika
hili simzungumzii Jaydee peke yake, nazungumzia wasanii wote wa Tanzania
nawazungumzia kuelewa kwamba tunajisahau sana.
Tunapata hela nyingi sana,
sitashangaa miaka mitatu baada ya leo, Ommy Dimpoz naye ukamsikia
anaandika hivi hivi, au Diamond naye ni kwasababu hakujipanga tu.”
Kuhusu shutuma kuwa Clouds FM inaua
muziki wa Bongo Flava, Ruge amesema, “inanishangaza kidogo kwasababu
Clouds inategemea matangazo ya biashara kwa asilimia 95, ndio biashara
yake hiyo.
Lakini inategemea muziki wa Bongo
Flava kama maudhui ya kipindi, inaanzaje kuuua, inategema wasanii wa
Bongo Flava kama wasanii wa kwenda kufanya shows mkoani.”
Kuhusu msimamo wa kampuni Ruge amesema:
Msimamo wa kampuni ni kwamba tunaamini kabisa mwanadada kinara wa muziki wa Tanzania naamini atakaa na kutafakari la kufanya.
Tunamtakia kila lakheri kwenye show
yake ya tarehe 31 afanye vizuri lakini atakapokuwa tayari sisi tuko
tayari kuendelea kufanya kazi, anajua cha kufanya.
0 comments:
Post a Comment