Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Wednesday, December 4, 2013

FAHAMU JINSI MAMILIONI YANAVYOTUMIKA ILI KUPANGA MATOKEO YA SOKA

FAINALI za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwakani zipo kwenye hatari kubwa ya kukosa mvuto. Ni kwa sababu kuna baadhi ya mechi matokeo yake yatapangwa na wacheza kamari, imeelezwa.

Wiki iliyopita watu sita walitiwa nguvuni kwa madai ya kushiriki kwenye kucheza kamari za kupanga matokeo ya mechi za soka na mmoja wa watuhumiwa hao alifichua kwamba mipango imeshawekwa tayari kwa ajili ya fainali zijazo za Kombe la Dunia na kwamba timu zote za Afrika zilizofuzu fainali hizo zipo kwenye himaya yake.

Timu za Afrika zilizofuzu ni Ghana, Ivory Coast, Nigeria, Cameroon na Algeria.

Hii ina maana kwamba atajipangia matokeo na mambo anayotaka yatokee kwenye mechi zao ili kushinda mamilioni ya kamari anayocheza.

Kwenye orodha ya waliotiwa nguvuni ni straika wa zamani aliyetesa kwenye Ligi Kuu England, Delroy Facey, ambaye kwa sasa ni wakala wa soka.

Facey, 33, aling’ara katika timu za Bolton Wanderers na Hull City zilipokuwa kwenye Ligi Kuu England kabla ya kufanya shughuli za uwakala wa soka.

Watu wengine waliokamatwa kwa kupanga matokeo ni Chann Sankaran, 33, kutoka Singapore na Krishna ­Ganeshan, 43, mwenye uraia wa nchi mbili; Uingereza na Singapore.

Wote walitarajiwa kufikishwa mahakamani jana Ijumaa. Kwa maelezo ya watu hao, Asia imeathirika zaidi kuwa na idadi ya watu wengi wanaoshiriki kwenye kupanga matokeo ya mechi za soka zinazochezwa duniani kote.

Kamari za upangaji wa matokeo ni virusi vinavyoishambulia soka kwa kiwango kikubwa kutokana na kuwashirikisha wahusika wenyewe kuanzia wamiliki wa timu, wachezaji, waamuzi na mawakala wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) wanaohakikisha wanatengeneza njia nzuri za mawasiliano ili kupanga matokeo ya mchezo.

Mambo yanavyofanyika

Kwa mujibu wa maelezo ya mtu huyo aliyenaswa, ni kwamba kinachofanyika katika kupanga matokeo kwa baadhi ya timu za klabu, wamiliki wake wamekuwa wakipigiwa simu usiku wa kuamkia siku ya mechi na kupewa maagizo kwamba lazima wafungwe kwenye mechi yao, huku hongo zikifanyika pia kwa makipa ili wafungwe kinafiki, mabeki wasababishe penalti kizembe kwa kushika mpira kwa makusudi huku mabao mengi ya dakika za mwishoni mwa mchezo yadaiwa kutokana na michezo hiyo ya kamari.

Kuna kundi jingine pia linalowahusisha wachezaji moja kwa moja wanaojiingiza kwenye upangaji wa matokeo kwa sababu jambo hilo linawaingizia pesa za ziada ukiacha mishahara yao na bonasi nyingine.

Nchi zinazoathirika

Ligi Kuu England kinachoinusuru ni mishahara mikubwa wanayolipwa wachezaji, lakini kwa nchi kama za Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Finland, Sweden na nchi mbalimbali za Afrika kuna wachezaji wanaoshawishika kirahisi na kukubali kucheza kamari hizo za kupanga matokeo.

Vikundi vinayojishughulisha na kamari hizo za kupanga matokeo vimekuwa vikitengeneza mazingira ya kuwasiliana na wachezaji, makocha au waamuzi ili kuhakikisha wanafanya kile wanakitaka wao ikiwa pamoja na kutoa kadi za njano, kadi nyekundu, kutoa penalti au kuhakikisha mechi husika inamalizika kwa matokeo ya sare.

Kadi ya njano yanunuliwa Pauni 5,000

Kwenye kamari hizo, kadi za njano zinazotoka ndani ya dakika 10 za kwanza kwa mchezaji ambaye alikubali kufanya tukio hilo zinamhakikishia mhusika kulipwa Pauni 5,000.

Lakini, mtu anayejihusisha na kamari hizo anasema kama mchezaji husika atashindwa kufanya tukio litakalomfanya aonyeshwe kadi ya njano ndani ya dakika 10 za mwanzo, basi atakuwa amepoteza nafasi ya kulipwa pesa hizo na hata kama ataonyeshwa kadi baada ya dakika hizo kupita, atakuwa yupo nje ya makubaliano.

Anasema: “Kwa mfano, ndani ya dakika 10 kama nitataka mchezaji aonyeshwe kadi ya njano na kadi moja ya njano thamani yake ni Pauni 5,000.

Hivyo ndivyo nilikuwa nikipanga na wachezaji. Kama hakutakuwa na kadi ya njano dakika hizo, hakuna malipo.”

Pauni 20,000 zanunua waamuzi

Kiasi cha Pauni 1.73 milioni zinatajwa kutumika kuwahonga wanaotumika kwenye kupanga matokeo kwa Ujerumani peke yake, wakati wachezaji kwenye nchi za Uingereza wamekuwa wakihitaji Euro 60,000 ili kukubali kucheza kamari hizo.

Kwa maelezo yaliyopatikana ni kwamba Pauni 20,000 zinatumika kumnunua refa anayechezesha mchezo husika ili apange matokeo wanayoyataka yaliyopangwa kwenye kamari zao, kwa mfano kwamba lazima mchezaji fulani aonyeshwe kadi ya njano au nyekundu.

Mwamuzi wa Armenia, Andranik Arsenyan, alifungiwa maisha baada ya kugundulika kujaribu kupanga matokeo ya mchezo wa Europa League wakati mwaka 2010, mwamuzi wa Bosnia, Novo Panic, pia alifungiwa maisha. Chann Sankaran na Krishna Sanjey Ganeshan, walitiwa mbaroni kwa kudaiwa kupanga matokeo kwenye mechi za England.

Serie A yachafuka zaidi

Wakati timu za Afrika zikidaiwa kuwekwa kwenye mchakato wa kupanga matokeo kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwakani na kutishia kupunguza uhondo wa michuano hiyo, Ligi Kuu Italia (Serie A) inaripotiwa kuchafuka zaidi kwa upangaji matokeo.

Ukiacha kashfa ya Calciopoli iliyosababisha Juventus kushushwa daraja mwaka 2006 kutokana na kupanga matokeo, lakini soka la Italia linaonekana kuoza kwa upangaji wa matokeo kwa sababu tukio hilo liliripotiwa kutokea tena mwaka 2011.

 Februari mwaka huu, BBC Sport ilitoa ripoti iliyoshitua wengi kwamba zaidi ya mechi 680 za soka duniani kote zimepangiwa matokeo, ikiwamo za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizofanyika England kati ya mwaka 2009 hadi 2013.

Zaidi ya nusu ya mechi hizo ni za Ulaya, huku Afrika na Asia ni mechi 300 zilizopangiwa matokeo.

Sunday, November 24, 2013

Kapuya akimbia nchi


SIKU moja baada ya binti anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kufungua jalada polisi dhidi yake, inadaiwa mbunge huyo ametoweka nchini...
 
Vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na mbunge huyo, vinadai kuwa amesafiri juzi kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.
 
Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini Sweden miezi miwili hadi mitatu.
 
Hata hivyo haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kumtuliza na upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.
 
Wakati Profesa Kapuya anakimbilia nje ya nchi, tayari alishafunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi.
 
Mtoa taarifa wetu anasema muda mchache baada ya Kapuya kushindwa kumshawishi binti huyo asimfungulie kesi ya ubakaji, wala kuogopa vitisho vya kuuawa, au kupokea pesa kiasi chochote aondoke nchini, Kapuya mwenyewe alipanga safari ya dharura na kwenda nje ya nchi.
 
Tanzania Daima  lilifanya juhudi za kuwasiliana na ofisi ya Bunge kujua kama wana taarifa zozote za kuondoka kwa mbunge huyo kwenda nje ya nchi na kujua ni sababu zipi hasa zimempeleka huko, lakini simu ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai ilikuwa inaita bila kupokelewa.
 
Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila naye hakupatikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) hakuujibu.
 
Hata hivyo, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu ambayo Kapuya ni mjumbe wake haina safari ya Sweden.
 
Tangu Tanzania Daima lianze kuandika tuhuma hizi nzito, kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi.
 
Harakati za kufungua jalada dhidi ya Kapuya zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.
 
Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.
 
Polisi wanena
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake zitathibitika.
 
Alisema Jeshi la Polisi lina mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
“Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na kurejeshwa kwao.
 
“Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana na hatufanyi kazi kinyume na taratibu zetu,” alisema.
 
Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya huku akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake.
 
Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.
 
“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.

Source: Tanzania Daima

Thursday, November 21, 2013

Sababu za Adan Rage kusimamishwa Adan Rage wazijua?Zisome hapa..Uongozi umezifafanua zaidi.

Jana uongozi wa klabu ya Simba ulitangaza kumsimamisha mwenyekiti wake Ismail Aden Rage.
Maamuzi hayo yalitokana na kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika hapo juzi,
Hizi ni Miongoni mwa sababu zilizotolewa kwenye mkutano wa waandishi wa habari zilizopelekea kusimamishwa kwa Mheshimiwa Rage.
Mkataba na AZAM  TV
Rage alisaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya kipindi ya cha Simba TV bila kuishirikisha kamati ya utendaji.
Wakati Rage anasaini mkataba na Azam TV tayari klabu ya Simba ilikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho kuingia mkataba na kampuni ya ZUKU kwa ajili kipindi cha Simba TV uliokuwa na thamani ya dola za kimarekani 300,000 kwa mwaka.
Kampuni ya ZUKU ilipokuwa kwenye majadiliano na viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga jijini Nairobi, kwenye mkutano huo Simba iliwakilishwa na Mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph Itang’are maarufu kama mzee Kinesi pamoja na mwanachama Evans Aveva wakati Yanga iliwakilishwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga na Francis Kifukwe,viongozi hao Simba Ghafla walisikia Rage kasaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya Simba TV.
Sakata la uhamisho wa Emmaanuel Okwi.
Mheshimiwa Rage ndiye aliyesimamia uhamisho wa mchezaji Okwi on CREDIT bila kuishirikisha kamati ya utendaji,matokeo yake klabu hiyo mpaka leo imeshindwa kupata pesa ya uhamisho wa mchezaji huyo.
.
Kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji.
Sababu nyingine iliyoelezwa ni kitendo chake cha kushindwa kuitisha vikao vya kamati ya utendaji, Kuendesha klabu na kufanya maamuzi binafsi bila ya kushirikisha kamati hiyo ya utendaji ambayo ilichaguliwa na wanachama
Strategic plan ( Mpango mkakati )
Hivi karibuni klabu ya Simba ilizindua mchakato wa kutengeneza mpango mkakati (Strategic Plan) lakini cha kushangaza mwenyekiti amekuwa hataki kuona mpango huo ukifanikiwa.
Mkutano mkuu wa katiba

Kushindwa kuitisha mkutano wa marekebisho ya katiba,kuchukua maamuzi binafsi ya kuhairisha mkutano maalumu wa katiba uliotakiwa kufanyika Novemba, mwaka huu.

Vichwa vya habari vya magazeti ya leo Alhamisi tarehe 21 November 2013

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.


                           Source;millardayo.com

BABU SEYA KULIA AU KUCHEKA LEO?

MAHAKAMA ya Rufani leo inatarajia kutoa uamuzi wa ama kulikubali au kulikataa ombi la marejeo lililowasilishwa na mwanamuziki wa dansi nchini, Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae, Papi Kocha ‘Mtoto wa Mfalme’, ambao waliomba mahakama hiyo ifanyie marejeo hukumu ya kifungo cha maisha iliyoitoa Februari 2010, kwa kuwa ina dosari za kisheria na kuwaachia huru.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa mahakama iliyotolewa kwa mawakili wa pande zote mbili, mahakama imemtaka Babu Seya na mwanae pamoja na mawakili wa pande zote kufika leo mahakamani ili wapokee uamuzi wa maombi hayo.

Oktoba 30 mwaka huu, jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk, walisikiliza ombi hilo lililowasilishwa mahakamani hapo na wakili wa waomba rufani, Mabere Marando.

Wakili Marando alidai kwa mujibu wa kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009  inatoa mamlaka kwa Mahakama ya Rufaa kufanya mapitio  ya hukumu inazozitoa,  hivyo wateja wake wamewasilisha ombi hilo kwa sababu wanaamini  mahakama ilikosea kisheria katika hukumu yake Februari 2010.

“Waheshimiwa majaji, kwa sababu jopo lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi  kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi wa watoto waliodai walitendewa vibaya na waomba rufaa (Babu Seya na Papii) na sheria za nchi zinasema endapo mahakama itabaini kuwa mahakama ya chini ilikiuka taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto wadogo, basi ushahidi ule wa watoto wadogo uliotumika katika mahakama ya chini kuwatia hatiani washitakiwa unafutwa na waomba rufaa au washitakiwa wanaachiwa.

“Nafahamu ni kazi ngumu kuwashawishi nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februari 2010, ambapo uliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa utetezi huo wa kisheria niliouainisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na hoja yangu kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi wa watoto wadogo, naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria na leo naiomba mahakama iwaachie huru wateja wangu,” alidai Marando.

Mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP), Angaza Mwipopo, Jackson Mlati, Imaculata Banzi na Joseph Pande, waliomba mahakama itupilie mbali ombi hilo, kwa kuwa sababu zote alizozitoa alizieleza wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamuliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februari mwaka 2010.

Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari, angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na si ombi lake kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu hiyo ambayo anadai ina dosari.

Source;TANZANIA DAIMA

Wednesday, October 2, 2013

Cheki Mwonekano mpya wa Agness Masogange baada ya kumaliza kesi yake Sauzi

Pichani juu ni taswira mbalimbali za muonekano mpya wa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ambaye kwa sasa yupo uraiani baada ya kufutiwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Sunday, September 22, 2013

Al shabaab wajitapa na kudai wameua wakenya 100 jana...Twitter wafunga account yao..


Zaidi ya watu 39 wameuawa na wengine 150 kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuliteka jengo lenye maduka la Westgate, jijini Nairobi, Kenya.

Tukio hilo lilitokea jana mchana ambapo watu waliokuwa wakizungumza lugha ya kigeni, inayodhaniwa kati ya Kiarabu au Kisomali, kuvamia jengo la ghorofa na kushambulia watu kwa risasi.


“Hawakuwa wakizungumza Kiswahili. Walikuwa wakizungumza kwa lugha kama vile Kiarabu au Kisomali, lakini sina hakika sifahamu lugha hizo,” alisema mmoja wa mashuhuda aliyefanikiwa kutoka ndani ya jengo hilo na kujitambulisha kwa jina moja la Jay.


Shuhuda mwingine aliyejitambulisha ni mfanyakazi wa Ubalozi wa Uholanzi jijini Nairobi, Rob Vandijk, alisema tukio hilo lilitokea wakati akipata chakula cha mchana ndani ya jengo hilo.


Alisema watu hao waliingia ndani ya jengo la maduka hayo 
na kuanza kushambulia watu kwa risasi.


Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu, Abbas Guled alisema: “Ninachoweza kusema tuna takriban maiti 20. Majeruhi ni wengi.”


Katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja baadaye, Rais Uhuru Kenyatta alithibitisha kuwa zaidi ya watu 39 walikufa katika shambulizi hilo la kinyama, na wengine 150 kujeruhiwa.


"Vyombo vya usalama vinafanya kila jitihada kuthibiti eneo hili na kuwakamata waliohusika," asema Mr Kenyatta, akiongeza kuwa naye pia amepoteza wanafamilia katika tukio hilo. 
 
Polisi Waingia

Taarifa zingine zilisema kuwa polisi waliwasili eneo la tukio dakika 30 baada ya watu hao kuvamia jengo hilo.


Kamanda wa Polisi wa Kenya, Inspekta Jenerali David Kimaiyo alisema kwamba polisi walifika katika jengo hilo baada ya kupata taarifa, ambapo nao walianza kujibizana kwa risasi na magaidi hao waliokuwa hapo ndani.


Alisema watu hao wanaosadikiwa ni magaidi walikuwa wakijaribu kuiba pesa katika jengo hilo, kabla ya polisi hawajatokea na kuanza kurushiana risasi.

Helikopta za polisi zilionekana zikilizunguka jengo hilo kwa juu kuhakikisha hakuna mhalifu yeyote ambaye anaweza kutoroka.


Mashuhuda walisema kwamba walikuwa wakipata chakula cha mchana jirani na jengo hilo, ghafla wakashuhudia milio wa risasi kutoka katika eneo hilo.

Polisi walifanikiwa kuingia katika jengo hilo baada ya kukaa kwa muda mrefu kuangalia namna ya kuingia kwa sababu hawakujua watu hao walikuwa wamejificha eneo gani.

Baada ya polisi kuingia katika jengo hilo watu waliokuwa ndani walipata fursa ya kutolewa, huku polisi wengine wakiendelea kuwatafuta wahalifu hao.

Al-Shabab Yanena
Wakati shambulizi likiendelea jana jioni, wanamgambo wa kikundi cha Kiislamu cha Al-Shabab walivyambia vyombo vya habari kupitia Twitter kuwa wamehusika na tukio hilo.

“Tulishaionya serikali ya Kenya kuwa dhahama itaikumba kama isipoondoa vikosi vyake kutoka Somalia,” Al-Shabab waliandika kupitia akaunti yao ya Twitter inayoitwa @HSM_Press.


Wanamgambo hao waliongeza kuwa wamefanikiwa kuua watu wengi  ( 100 ) kuliko idadi inayotajwa na serikali ya Kenya, huku wakibeza jitihada za uokoaji.

Kutokana na malalamiko kutoka kwa waathirika wa tukio na vyombo mbalimbali vya usalama, FastCompany inaripoti kuwa Twitter ililazimika kuifunga akaunti hiyo  usiku  wa  kuamkia  leo.

HIZI  NI  TWEET  ZAO  KATIKA  ACCOUNT  YAO  NYINGINE  MAANA  WANAZO  KAMA  3  ivi:

 

PICHA ZA KUSIKITISHA KATIKA SHAMBULIO LA KENYA HAPO JANA..!! TAHADHARI BAADHI YA PICHA ZINATISHA.!


September 21, ni tarehe ambayo Kenya haitoisahau kamwe. Ni baada ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabab lilipoishambulia mall ya Westgate maarufu kwa kuwa na wateja matajiri jijini Nairobi na kuwashikilia watu mateka, kuwaua na kuwajeruhi wengine.
Mwanamke aliyekuwa amejeruhiwa akiomba msaada Mwanamke aliyekuwa amejeruhiwa akiomba msaada
Familia ikiwa imeshikana mikono wakati ikitoka nje ya eneo la hatari Familia ikiwa imeshikana mikono wakati ikitoka nje ya eneo la hatari
article-2427892-182485E800000578-152_964x631
130921145130-25-kenya-mall-restricted-horizontal-gallery
130921103725-07-kenya-mall-horizontal-gallery
Mashuhuda wanasema watu hao waliokuwa na silaha, wakiwa na nguo nyeusi na vichwa vyao vikifunikwa na vilemba waliingia kwenye mall hiyo ya Westgate jana mchana. Mpaka sasa, idadi ya watu walioshikiliwa mateka ndani ya mall hiyo haijajulikana.
Mama na wanae akiwa amejificha kuhofia kuuawa na watu hao makatili Mama na wanae akiwa amejificha kuhofia kuuawa na watu hao makatili
Mfanyakazi wa Red Cross akimbeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyo Mfanyakazi wa Red Cross akimbeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyo
Mtoto akikimbia kuokoa maisha yake Mtoto akikimbia kuokoa maisha yake
Mtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa
Mtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa

Zaidi ya watu 40 wameripotiwa kuuawa na zaidi ya 162 wakijeruhiwa.
Mtu na mpenzi wake waliouwa kwa pamoja na wanamgambo hao Mtu na mpenzi wake waliouwa kwa pamoja na wanamgambo hao
Mwanamke akilia kwa woga baada ya kuokolewa na askari Mwanamke akilia kwa woga baada ya kuokolewa na askari
Mwanamke aliyejeruhiwa akitolewa nje kwa kubebwa kwenye toroli la kufanyia shopping Mwanamke aliyejeruhiwa akitolewa nje kwa kubebwa kwenye toroli la kufanyia shopping
Mwanamke aliyekuwa ameshikiliwa mateka akiwa haamini baada ya kuachiwa Mwanamke aliyekuwa ameshikiliwa mateka akiwa haamini baada ya kuachiwa
Maafisa wamesema watu hao wamebananishwa na kwamba watu wameshikiliwa mateka kwenye maeneo mbalimbali. Al-Shabab imeliambia shirika la habari la Uingereza BBC kuwa limefanya shambulio hilo kujibu opereshini za kijeshi za Kenya zinazoendelea nchini Somalia.
<img src="http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/09/Mwanaume-aliyejeruhiwa-akilia-kwa-uchungu-kutokana-na-maumivu-makali-baada-ya-kupigwa-risasi-ya-mguu.jpg" alt="Mwanaume aliyejeruhiwa akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali baada ya kupigwa risasi ya mguu" width="600" height="400" class="aligncenter size-full wp-image-57459" Mwanaume aliyejeruhiwa akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali baada ya kupigwa risasi ya mguu
Ofisa wa usalama na wenzake wakielekezana na wenzake mahali walipo watu hao wenye silaha Ofisa wa usalama na wenzake wakielekezana na wenzake mahali walipo watu hao wenye silaha
Polisi akisaidia kumtoa mtoto aliyekuwa ndani ya mall Polisi akisaidia kumtoa mtoto aliyekuwa ndani ya mall
Polisi na wanajeshi wakipambana na magaidi hao Polisi na wanajeshi wakipambana na magaidi hao
Mashuhuda wengine wamedai kuwa wanamgambo hao waliwaambia waislamu waondoke na wabaki waumini wa dini zingine.
“Walisema na kusema: ‘Kama wewe ni muislamu, simama. Tumekuja kuwaokoa,” Elijah Lamau aliiambia BBC. Alisema waislamu waliondoka wakiwa wamenyoosha mikono juu na kisha watu hao wakawapiga risasi watu wawili.
Polisi wa Kenya akiwa ameshika tumbo lake baada ya kujeruhiwa huku mwenzake akiendelea kurushiana risasi na magaidi wa Al-Shabab Polisi wa Kenya akiwa ameshika tumbo lake baada ya kujeruhiwa huku mwenzake akiendelea kurushiana risasi na magaidi wa Al-Shabab
Polisi wakiingia ndani ya mall hiyo kupambana na wana mgambo wa Al-Shabab Polisi wakiingia ndani ya mall hiyo kupambana na wana mgambo wa Al-Shabab
Polisi wakipambana na Al-shabab Polisi wakipambana na Al-Shabab
Rais wa Canada Annemarie Desloges, 29, aliuawa kwa risasi na magaidi hao Raia wa Canada Annemarie Desloges, 29, aliuawa kwa risasi na magaidi hao
Wanajeshi walimwaga kwenda kusaidia kupambana na watekaji wa kundi la kigaida la Al-shabab Wanajeshi walimwaga kwenda kusaidia kupambana na watekaji wa kundi la kigaida la Al-Shabab
Wananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiwambia kuinua mikono yao kuonesha hawana silaha Wananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiwambia kuinua mikono yao kuonesha hawana silaha
Gaidi mmoja alikamatwa jana na kufa kutokana na majeraha. Maafisa wa Kenya wameimbia BBC kuwa wengine wanne wamekamatwa. Wananchi wakikimbia kuokoa maisha yao Wananchi wakikimbia kuokoa maisha yao
Wanawake na watoto wao wakihaha kuokoa maisha yao ndani ya mall hiyo Wanawake na watoto wao wakihaha kuokoa maisha yao ndani ya mall hiyo
Wanawake waliojeruhiwa wakisaidiwa Wanawake waliojeruhiwa wakisaidiwa
Watu mbalimbali wakijaribu kuokoa maisha yao wakati watu hao wenye silaha wakiwa ndani ya mall Watu mbalimbali wakijaribu kuokoa maisha yao wakati watu hao wenye silaha wakiwa ndani ya mall
Watu wakimsaidia kumdaka msichana aliyekuwa amejificha ndanii ya mall hiyo Watu wakimsaidia kumdaka msichana aliyekuwa amejificha ndanii ya mall hiyo
Watu wakisaidiwa kutoka nje ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa Watu wakisaidiwa kutoka nje ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa
Watu waliokuwa ndani ya Westgate wakisaidiwa kutoka nje na askari Watu waliokuwa ndani ya Westgate wakisaidiwa kutoka nje na askari
Watu waliokuwa wakifanya shopping wakisaidiwa kutoka nje ya mall na askari Watu waliokuwa wakifanya shopping wakisaidiwa kutoka nje ya mall na askari

Source: Bongo5