Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Wednesday, May 22, 2013

Rais Obama kutua Tanzania Julai Mosi


Wakati Ikulu ya Marekani ikitangaza kuwa Rais Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu kuanzia Julai Mosi hadi 3, Serikali ya Tanzania imesema ujio huo utasaidia kuinua uchumi kutokana na kufaidika na uwekezaji na misaada mbalimbali. 
Rais Obama anatarajiwa kuzitembelea Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Taarifa ya Ikulu ya Marekani iliyotolewa na Ubalozi wa nchi hiyo nchini, inasema Rais Obama atazuru Afrika kuanzia Juni 26 hadi Julai 3, ikiwa ni moja ya sehemu ya kuimarika uhusiano baina ya nchi yake na bara la Afrika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma alisema ziara ya kiongozi huyo inatarajiwa kuinufaisha Tanzania maeneo ya biashara na uchumi.
Rais Obama ambaye ana asili ya Kenya ambako anatoka baba yake mzazi, baada ya kuchaguliwa kushika madaraka nchini mwaka 2009, alimwalika Rais Kikwete akiwa kiongozi wa kwanza kwenda Marekani kujadiliana masuala mbalimbali.
Ziara yake ya kwanza kwa bara la Afrika aliifanya nchini Ghana ambako alihutubia Bunge.

0 comments:

Post a Comment