Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Saturday, April 20, 2013

WAZAZI WENGINE MH!!! BABA KANUMBA ASEMA HANA ULAZIMA WA KULIONA KABURI LA KANUMBA!!

Stori:Gladnees Mallya
BABA wa marehemu Steven Kanumba, mzee Charles Kanumba amefunguka kuwa haoni ulazima wa kuliona kaburi la mwanaye na kuhusu kufanya maombi mwaka mmoja baada ya kifo, alifanya akiwa huko nyumbani kwake Shinyanga.
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu hivi karibuni, mzee Charles alisema mtu anapofariki kikubwa ni kuombewa na hilo la kwenda kulitazama kaburi lake haliwezi kuwa na faida.
“Mimi nilifanya sala ya kumuombea Kanumba pamoja na mtoto wa dada yake ambaye walikufa kwa kufuatana kwenye Kanisa la AIC Shinyanga,” alisema mzee huyo na kuongeza;
“Mtu akishakufa kinachobaki ni kumuombea huko aliko na kaa ukijua kwamba huku ndiyo kwenye chimbuko la marehemu hivyo nisingeweza kwenda kufanyia maombi kwenye mji mwingine.”

Chanzo:www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment