Kweli sikio la kufa halisikii dawa! Licha kuolewa na Sunday Demonte,
msanii wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel ametia aibu kwa mara nyingine
tena baada ya kunaswa nusu utupu ukumbini usiku wa manane, Risasi
Jumamosi linafunguka.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilijiri juzikati katika
Ukumbi wa Nyumbani, mjini hapa ambapo Aunt aliwashangaza mashabiki
waliofurika kwenye shoo ya Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
Aunt alivaa kipensi kilichoacha mapaja yote wazi hadi kulazimika
kujifunika kwa pochi na kitopu ‘transiparenti’ kilichoonesha kila kitu
hadi ‘chakula ya mtoto’.
Baada ya midume kumuona akiwa amevaa kihasara huku akijificha nyuma ya
jukwaa baadhi yao walimfuata na kuanza kumzingira kisha kumwagizia ulabu
kama mvua kila mmoja akitamani kuondoka naye kwenda kumfaidi kimapenzi.
Baadhi ya madalali wa magari wa eneo la Masika mjini hapa walimvamia
Aunt na kuanza kumgombea wakiongozwa na mmoja wao aliyeonekana kuwa
jirani zaidi na msanii huyo.
Mwanahabari wetu alipomfuata Aunt na kumuuliza kulikoni akatoka Dar
kuwafuata Ngwasuma Mji Kasoro Bahari huku akiwa kihasara kiasi hicho,
mke huyo wa mtu alifunguka: “Nipo hapa Moro zaidi ya siku sita na
nitaendela kuwepo kwa zaidi ya siku kumi, nipo na kundi langu tunarekodi
filamu kwenye Hoteli ya Nashera.”
Alipobanwa kuhusiana na kinguo alichovaa huku mapaja na maungo mengine
nyeti yakionekana, alicheka na kukatisha mahojiano: “Siwezi kuzungumza
chochote kama vipi chukua namba yangu unipigie kesho.”
Kesho yake alipopigiwa, simu yake iliita bila kupokelewa.
Siyo mara ya kwanza, Aunt amekuwa akifanya matukio yasiyoendana na hadhi
ya mke wa mtu akijiachia kihasara ikiaminika kuwa anafanya hivyo kwa
kuwa hakai na mumewe ambaye yupo huko Dubai.
0 comments:
Post a Comment