KUTOKANA na kuchakaa haraka kwa noti ya shilingi 500 na kiwango chake
kudumu kwenye mzunguko kwa miezi sita tu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
imesema inatarajia kubadili noti hiyo na kuwa ya sarafu.
Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima juzi kwenye viwanja vya
maonesho ya kimataifa ya biashara, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo
cha Fedha, Abdul Dollah, alisema mabadiliko hayo yatafanyika hivi
karibuni na sarafu hiyo itadumu kwenye mzunguuko kwa zaidi ya miaka 20
huku ikiwa na ubora wake.
Dollah alitaja sababu nyingine ya uchakavu huo ni kutokana na noti hiyo
kushikwa na watu wengi kwenye mzunguko huku baadhi yao wakishindwa
kuzihifadhi vizuri:
“Tofauti na noti nyingine kama vile zile za sh 5,000 na 10,000 hizi
utakuta mara nyingi uchakavu wake si kama ule wa sh 500 kwa sababu noti
hizi watumiaji wake wengi ni wale wenye akaunti benki.”
0 comments:
Post a Comment