Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Saturday, July 20, 2013

Kitale, H.Baba na Dogo Janja waungana na wananchi kwa pamoja kupinga kodi ya Simcard


Baada ya serikali kupitisha sheria ya kuanzishwa kwa tozo ya Tsh 1000 kwa mwezi kwa kila kadi ya simu ya mkononi, wananchi wengi wamejitokeza kuipinga kwa madai kuwa itamkandamiza mwananchi wa kawaida. Dogo Janja, H.Baba na Kitale nao wameungana na wananchi wengine kuipinga kodi hiyo.

“Serikali ina vyanzo vingi vya mapato, kwanini wanataka kutunyonya Watanzania badala ya kufanya vitu vingine ili serikali ipate mapato bila kuathiri maisha ya Watanzania,” anahoji Dogo Janja. Wanang’ang’ania kadi za simu kwa hali hii wataathirika watu wa vijijini ambao hawana vipato vya uhakika. Maoni yangu kwa serikali ijipange na kutafuta vyanzo vingine vya mapato.”

Naye H.Baba alisema, “Siyo haki wangepandisha bia na sigara siyo kadi za simu, ila ndiyo serikali yetu hiyo ni miradi ya watu binafsi sio serikali , swala letu la wasanii kuibiwa kazi zetu limewashinda.”.

“Katika Watanzania wote sio wote wana uwezo wa kumiliki simu zao,” anasema Kitale. Kuna wengine hata pesa ya kununulia vocha hawana wao nikupigiwa na kubeep, hatuoni wanaongezewa mzigo ambao utasababisha mwisho wa siku hata simu zenyewe ziwekwe chini ya kitanda.”

Ameongeza, “Hebu angalia swala la mawasiliano ni haki yako ambayo kwa sasa linakuwa ni biashara kwa watu fulani ,tunanunua simu ,tunanunua line,tunachaji kibandani kwa pesa,tunanunua vocha kwaajili ya mawasiliano bado tena tunaongezewa mzigo wa kulipia line ya simu kwakweli serikali ijaribu kutafuta vyanzo vingine vya mapato.”


0 comments:

Post a Comment