Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Thursday, June 13, 2013

Vitendo vya Ushoga vyazidi kuenea Bongo,hawa wengine tena wakamatwa wakibanjuana.Soma full story hapa

Tukio hilo lililoshuhudiwa na watu kibao,
lilijiri Juni 10, mwaka huu katika nyumba
moja ya kulala wageni iliyopo Kinondoni jijini
Dar.
Kunaswa kwa wanaume hao ambao ilidaiwa
walikuwa kwenye harakati za kufanya
Usodoma na Ugomora, kulifuatia mke wa
mmoja wao kunasa meseji za kimapenzi
walizokuwa wakitumiana wawili hao.
Mama huyo alipobaini meseji hizo chafu,
wawili hao wakisisitiziana kukutana kwenye
gesti hiyo usiku wa siku hiyo, alimpigia simu
mmoja wa waandishi na  kumpa mkasa
mzima ambapo walikubaliana saa moja
zoezi  la kuwanasa  litaanza..
Ilipofika saa 1:30 usiku, timu yetu, mama
huyo, wapambe wake na polisi walikuwa
wanafanya doria nje ya gesti hiyo.
Saa 5:30 usiku, mume wa mwanamke huyo
akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa shoga
walifika gesti hiyo bila kujua kama waliwekewa
mtego wa kunaswa na kwenda kuchukua
chumba namba 2.
Wakiwa ndani, mke alimpigia simu mumewe
na kuhoji alipokuwa akajibiwa alikuwa mitaa
ya nyumbani kwao Manseze, Dar akipiga stori
na rafiki zake.
Wawili hao wakiwa wanajiandaa na mchezo
wao usiofaa, polisi aligonga mlango akijifanya
mhudumu aliyetaka kumpatia taulo, jamaa
bila kujua alifungua ndipo walipofumaniwa na
kuibua varangati zito.
Kufuatia timbwili hilo, waliwekwa chini ya
ulinzi na kutolewa pale gesti tayari kupelekwa
kituoni ndipo mwanaume anayedaiwa kuwa
shoga akatimua mbio mithili ya mwanariadha
wa kimataifa, Usain Bolt wa Jamaika na
wanandoa hao waliendelea kuzozana huku
mke akimlalamikia mumewe na kumwambia
wakifika nyumbani ampe talaka yake.
Hata hivyo, mwanamke huyo aliomba sakata
hilo lisipelekwe polisi kwa madai alichotaka ni
kumfumania mumewe na kwamba alikuwa na
ushahidi wote.
GPL

0 comments:

Post a Comment