Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Friday, June 14, 2013

Huu ndo ukweli wenyewe kuhusiana na tukio la Masele kupata ajali.soma hapa...

Habari za uhakika ni kuwa muigizaji wa
vichekesho nchini maarufu kwa jina la
Masele cha Pombe ni mzima wa afya na
hajafariki kama baadhi ya tetesi
zilivyoanza kuenea kwa kasi.
Swahiliworldplanet baada ya kusikia tetesi
kuwa Masele amefariki kwa ajali ya gari
jioni hii huko Tanga ilibidi kutafuta ukweli
kuhusu muigizaji huyo maarufu na
kufanikiwa kupata habari za kina kupitia
Kabuti Onyango ambaye ni cameraman
maarufu wa filamu za kitanzania. Kabuti
ambaye ni mtoto wa Mzee Onyango
ambaye ni muigizaji mkongwe
nchini amesema kuwa amezungumza na
baba yake(Mzee Onyango) muda mfupi
uliopita ambaye yupo Tanga na jibu ni hili
" baba yupo Tanga mzee onyango na nime
mpigia simu kaniambia kwamba walikuwa
na masele kwenye hilo gari lakini si
kwamba amefariki hapana ila masele
aligonga mtu akakamatwa na raia
wakavunja kioo na kutaka kumuua
aligonga mtu wa kwanza na akataka
kukimbia akagonga mwingine ndio ilivyo
kuwa lakini ni mzima na yupo kituo cha
police"

0 comments:

Post a Comment