Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Tuesday, June 4, 2013

Exclusive: Jokate aongea baada ya Diamond kukiri kuwa anajuta kumkosea na kuuvunja moyo wake

Hivi karibuni Diamond aliamua kuweka ‘ego’
pembeni na kukiri kuwa Jokate Mwegelo ndiye
msichana katika maisha yake aliyemkosea
sana na anajuta kumuumiza
Diamond alifunguka hayo kwenye kipindi cha
Take One cha Clouds TV, kilichorushwa wiki
iliyopita.
Akiongelea jinsi alivyomuumiza Jokate,
Diamond alisema, “Kwasababu alikuwa too
innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu
chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza
kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti
kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend
wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi,
nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa
niko naye halafu ghafla nikarudisha
mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu
still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga
hivi nasema nilimkosea.”
Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate,
Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui,
I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi
kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa
nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya
maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi
yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana,
halafu mtoto wa watu mstaarabu sana,
alijitahidi kujenga career yake sasa hivi
imekaa vizuri.”
Bongo5 imewasiliana na Jokate ili kutaka
kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli
ya Diamond aliyesema anafurahi kuona
Diamond amefunguka ukweli.
“Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad
kama ame-acknowledge I was innocent in that
whole matter,” amesema Jokate.

0 comments:

Post a Comment