Wadau natumain hamjambo,
Nina rafiki yangu ambaye ni kama ndugu,tumetoka mbali sana na sasa ni
kama mtu na kaka yake.jamaa yangu huyu(hajaoa) alikuwa na dem mmoja hivi
lakini walishindwana kwa matatizo yao binafsi wakawa wameachana kama
mwaka mmoja uliopita.
Kwa kuwa nilikuwa nishatambulishwa kwa shemej yangu huyo basi hata baada
ya kuachana na jamaa yangu tukawa tunasalimiana,iko siku ananipigia na
mimi kuna siku nampigia kumsalim. Tunaitana shemej.
Kuna kipindi shemej yangu huyo alikuwa na shida ya vijisent,kwa kuwa
hakuweza kumwambia ex wake basi aliniambia mimi lakini nilimtonya ex
kuwa mwenzake alikuwa na shida,jamaa hakutaka kumsaidia kabisa ex
wake,nikachukua jukumu la kumsaidia huyo shem wangu.basi mawasiliano
yakawa yapo kama kawaida kwa shem wangu huyo. Kuna siku shem aliniuliza
kama wyf yupo home,nikamwambia alikuwepo lakini keshaondoka kurudi
kazini kwake mkoa ana kama miez miwili sasa.
Basi shem akawa akinipigia simu hadi nyt kali kunisalimia na kunitakia
usiku mwema. Mwisho wa siku shem akaniuliza nawezaje kuishi muda wote
huo wakati wyf hayupo? Nikamjibu navumilia tu, akaniambia kweli huo ni
muda mrefu ila endapo nitakuwa na shida yoyote yuko tayar
kunisaidia,nanukuu;"nakuonea huruma shem wangu, muda huo ni mwingi sana
kwa mwanaume,endapo utahitaji kampani yangu niko tayar kukusaidia kwa
lolote wakati wyf hayupo,kwani hata huyo jamaa yako mi siko nae
tena,hata mimi nilishapata mtu mwingine japokuwa kwa sasa hayupo,atarudi
januari mwakani".
Niliingiwa na uoga sana lakini nikajikaza na kumwambia jamaa yangu kuwa
ex wake kanipa ofa ya kapani yake na niitumie nitakavyo, jamaa akanijibu
kuwa yeye alishamalizana nae, na hana sababu tena ya kurudiana nae,
kama nina uwezo wa kutumia ofa hiyo basi niendelee nayo.
wadau hiyo ndo situation niliyonayo kwa sasa,naomba mwenye ushauri mzuri zaid na wa manufaa anisaidie
0 comments:
Post a Comment