Kwa mara nyingine staa mkubwa wa
sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatengeneza kichwa cha habari
baada ya kuacha historia jijini Arusha kufuatia ulinzi mkali aliokuwa
nao, Ijumaa lina data zote.
Ilifahamika kuwa ndani ya ndege hiyo ambayo kuikodisha ni mkwanja mrefu, aliongozana na kampani yake tu.
Ilibumburuka kuwa timu yake hiyo
ilikuwa takriban watu watano ambao walimsindikiza kwenda kwenye
mapumziko kutokana na ‘stresi’ alizokuwa nazo.
Baada ya kutokea kwa ishu hiyo ndipo Wema alipoamua kwenda kujichimbia Arusha kupoteza mawazo.
Walipoingia jijini Arusha, staa huyo
wa Filamu ya The Super Star alipokelewa kwa ulinzi mkali hadi katika
hoteli ya bei mbaya aliyokuwa ameweka oda kwa ajili yake na watu wake.
“Unaambiwa kuanzia Arusha Airport (uwanja wa ndege) hadi hotelini ilikuwa ni full ulinzi wa kufa mtu,” kilisema chanzo chetu,
APOKEA MWALIKO
Habari zilieleza kuwa akiwa hotelini
hapo, habari zilienea kama moto wa kifuu kuwa yupo jijini Arusha hivyo
akapokea mwaliko kutoka kwa mashabiki wake waliotaka japo kumuona tu
kwenye Fashion Show iliyoandaliwa.
KASHESHE
‘Eventi’ ilifanyika kwenye Ukumbi wa
Club D (World Garden) uliopo jijini humo na ndipo kasheshe lilipoibuka
kwa watu kukanyagana wakitaka kumuona na kupiga naye picha.
“Aisee Wema wee acha tu! Kusema kweli
watu wanampenda sana. Kuna wakati niliona kama ukumbi unakuwa mdogo na
kwa taarifa yako ilikuwa haijatangazwa. Sijui kama ingekuwa imetangazwa
kuwa Wema yupo A-town, ingekuwaje maana kila mtu alitaka japo amshike
tu,” alisema sosi wetu huyo.
MENEJA
Kwa mujibu wa meneja wake, Martin Kadinda, ilibidi kuomba ulinzi maalum wa mabaunsa ambao walihakikisha hadhuriki.
“Tuliwaambia tupo na mtu mkubwa sana
hivyo tukapatiwa ulinzi maalum wa kuhakikisha Wema hapati tatizo la mtu
kumdhuru na ndicho tulichokifanya,” alisema Kadinda.
Ilifahamika kuwa kwa harakaharaka
ulinzi wa Wema ulikuwa na takriban watu wasiopungua 10, yote ikiwa ni
kuhakikisha usalama wake.
AFANANISHWA NA KIM KARDASHIAN
Kwa mujibu wa mashabiki wake ukumbini
hapo, ulinzi wa Wema ulifananishwa na ule wa staa wa Marekani, Kim
Kardashian ambaye hivi karibuni aliwekwa mtu kati na watu zaidi ya 32
wakiwemo askari na mabaunsa.
“Kweli Wema sasa amefikia levo za akina Kim, yaani naye ana ulinzi mkubwa hivi?” alihoji mmoja wa mashabiki wake.
TIMU NZIMA
Ukimwacha Wema na Kadinda, wengine
walioambatana nao ni Kajala Masanja, Petit Man ‘Wakuache’, Tinny Daddy
na Nurdin Bilal ‘Shetta’.
Baada ya mapumziko wote walirejea jijini Dar na kuendeleza libeneke wakiwa ‘wamerefreshi’ akili.
NI KUFURU NYINGINE
Hii ni kufuru nyingine ya Wema ambapo
swali liliendelea kubaki palepale kuwa anapata wapi fedha anazotumia
katika matukio yake ya gharama kubwa huku nyuma yake kukiwa na madai
kuwa kuna ‘mkubwa’ mmoja anamuwezesha
SOURCE: Global Publishers
0 comments:
Post a Comment