
Twitter pia hufanya hivi ili kukutofautisha na watumiaji wengine wanaoweza kutumia jina lako katika mtandao huo na wamekuwa wakifanya hivyo kwa watu maarufu katika nyanja mbalimbali kama muziki, serikali, siasa, uigizaji, dini, mitindo, uandishi wa habari, biashara n.k.
Ambwene Yesaya [@AyTanzania] amekuwa ni mwanamuziki wa kwanza kutoka Tanzania mkubwa anaeendelea kufanya vizuri duniani na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika tasnia ya muziki, for his twitter account to be verified amekuwa mmoja kati ya watanzania wachache ambao account zao zimekuwa hivyo akiwemo mcheza kikapu wa Oklahoma City Thunder(OKC) Hasheem Thabeet [@hasheemthedream], Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete [@jmkikwete] Flaviana Matata [@FlavianaMatata] na Waziri January Makamba [@jmakamba].
0 comments:
Post a Comment