September 21, ni tarehe ambayo Kenya haitoisahau kamwe. Ni baada ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabab lilipoishambulia mall ya Westgate maarufu kwa kuwa na wateja matajiri jijini Nairobi na kuwashikilia watu mateka, kuwaua na kuwajeruhi wengine.
Mashuhuda wanasema watu hao waliokuwa na silaha, wakiwa na nguo nyeusi na vichwa vyao vikifunikwa na vilemba waliingia kwenye mall hiyo ya Westgate jana mchana. Mpaka sasa, idadi ya watu walioshikiliwa mateka ndani ya mall hiyo haijajulikana.
Mtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa
Zaidi ya watu 40 wameripotiwa kuuawa na zaidi ya 162 wakijeruhiwa.
Maafisa wamesema watu hao wamebananishwa na kwamba watu wameshikiliwa mateka kwenye maeneo mbalimbali. Al-Shabab imeliambia shirika la habari la Uingereza BBC kuwa limefanya shambulio hilo kujibu opereshini za kijeshi za Kenya zinazoendelea nchini Somalia.
<img src="http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/09/Mwanaume-aliyejeruhiwa-akilia-kwa-uchungu-kutokana-na-maumivu-makali-baada-ya-kupigwa-risasi-ya-mguu.jpg" alt="Mwanaume aliyejeruhiwa akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali baada ya kupigwa risasi ya mguu" width="600" height="400" class="aligncenter size-full wp-image-57459" Mwanaume aliyejeruhiwa akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali baada ya kupigwa risasi ya mguu
Mashuhuda wengine wamedai kuwa wanamgambo hao waliwaambia waislamu waondoke na wabaki waumini wa dini zingine.
“Walisema na kusema: ‘Kama wewe ni muislamu, simama. Tumekuja kuwaokoa,” Elijah Lamau aliiambia BBC. Alisema waislamu waliondoka wakiwa wamenyoosha mikono juu na kisha watu hao wakawapiga risasi watu wawili.
Gaidi mmoja alikamatwa jana na kufa kutokana na majeraha. Maafisa wa Kenya wameimbia BBC kuwa wengine wanne wamekamatwa.
Source: Bongo5
0 comments:
Post a Comment