
“MSANII aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya
filamu nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya,
amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.
MAMBO yanaendelea kumwendea kombo mwigizaji huyo huku akiwa ameanza
kuporomoka vibaya kwenye sanaa na kujikuta akiingia matatani kwa tuhuma
za aibu.
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga
moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa
Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa
kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA
MAUNGONI.”
Katika kujibu tuhuma zilizoripotiwa na gazeti hilo, Uwoya kupitia
akaunti yake ya Instagram leo amepost picha ya ukurasa wa mbele wa
gazeti hilo wenye habari hiyo pamoja na maneno yafuatayo:
“Minimti wenye matunda milele siogop kupigwa mawe…shigongo kamua
kunichafua coz nakes nae mahakaman…anadhan ntaiacha never yeye aponde
anavyoweza ila mwisho wasiku sheria iatafata mkondo wake….minayake mengi
nayajua ila ngoja ninyamaze nisimwagiwe tindikali”
0 comments:
Post a Comment