Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Wednesday, June 26, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAR 26/6/2013

Tuesday, June 25, 2013

UJIO WA OBAMA DAR:ULINZI MKALI AIRPORT

Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini.
Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.
Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa.
“Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,” alisema Malaki.
Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali.
“Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.
Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.
Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Malaki alisema maofisa wa Marekani wanaowasili nchini wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kuwa hali ya usalama inaimarishwa na kuwaacha wazawa wakifanya shughuli za kawaida.

MOHAMMED DEWJI; Mtanzania wa kwanza kutokea kwenye frontpage ya jarida maarufu la Forbes Magazine

-Mo mjasirimali kijana mwenye mafanikio ya kipekee katika bara la Afrika.
Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.

Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.

Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.

Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
“Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 50 za kimarekani hadi dola Billioni 2.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.

Appreciation; Bongocelebrity.com

Wednesday, June 19, 2013

VURUGU ARUSHA: CHADEMA YAGOMA KUTOA USHAHIDI POLISI, LEMA AJIFICHA ....WAANDISHI WALA KICHAPO

                    Wabunge wanne wa Chadema, Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu) wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na mkusanyiko usio halali kwenye Uwanja wa Soweto jana.

Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jana kwamba pamoja na wabunge hao pia wamewakamata watu wapatao 60 kutokana na vurugu zilizozuka jana baada ya Polisi kuwatawanya kwenye uwanja huo waliokuwa wamekusanyika kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea kwenye uwanja huohuo, Jumamosi iliyopita.

Mbali ya viongozi hao, alisema wanawasaka Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

“Tunawasaka wabunge ili tuwajumuishe na watu hawa kwa kosa la kuhusika na mkusanyiko usiokuwa halali. Hadi sasa tumefanikiwa kulinasa gari la Mbowe,” alisema Chagonja.

Pia kamatakamata hiyo imemkumba Mpigapicha wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Ashraf Bakari. Polisi walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya waombolezaji hao.

Awali, Kamishna Chagonja alisema jana asubuhi kuwa wamelazimika kuzuia viwanja hivyo kutumika baada ya wamiliki wake, AICC kuzuia shughuli za Chadema kwenye eneo lao na kwamba upelelezi bado unaendelea katika viwanja hivyo.

Kamishna Chagonja aliwaonyesha waandishi wa habari barua aliyosema imeandikwa na uongozi wa AICC kuzua Chadema kuendelea kuutumia Uwanja wa Soweto.

Mabomu yarindima

Dalili za kuzuka kwa vurugu zilianza kuonekana asubuhi baada ya polisi kuzingira uwanja huo na kuzuia watu waliokuwa wameanza kufurika katika eneo hilo kuanzia saa moja kuingia kwa ajili ya maombolezo.

Wakati Polisi wakiwa uwanjani, wananchi walijaa nje ya uwanja na kuonekana kama wamewazingira.

Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe waliwasili uwanja hapo yapata saa nane mchana na kukuta zuio hilo na kuanza kuzungumza na wananchi ingawa FFU walikuwa wakiwataka watu kutawanyika. Mabomu yalianza kurindima wakati Arfi aliposimama na kuwahimiza wananchi kuelekea Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuaga miili ya marehemu.

“Tuna muda mfupi sana wa kuzungumza hapa, tunaomba wote tuelekee Hospitali ya Mount Meru kuaga miili ya marehemu kwa sababu uwanja huu umezuiwa na polisi,”alisema Arfi kabla ya kukatishwa na milipuko ya mabomu.

Awali, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema alitoa msimamo wa chama hicho kuwa Mwenyekiti wao, Mbowe na Lema hawatatoa ushahidi wa tukio la bomu wala kujisalimisha polisi kwa sababu hawana imani na jeshi hilo.

“Namtaka Chagonja atangulie mahakamani, tutakutana hukohuko. Mbowe na Lema hawatatoa ushahidi wala kujisalimisha polisi... ” alisema Lissu na kuongeza:

“Kisheria haiwezekani polisi ambao ndiyo watuhumiwa ndiyo wadai kukabidhiwa ushahidi ili wauharibu.”

Mapema Kamishna Chagonja aliwataka Mbowe na Lema kutoa ushahidi wa polisi kuhusika na tukio la kurusha bomu kwenye mkutano wa Chadema la sivyo polisi watatumia sheria kuwalazimisha kufanya hivyo.

Hekaheka

Baada ya polisi kuanza kutupa mabomu saa 8.45 mchana, wabunge, viongozi waandamizi wa Chadema na watu waliokuwa wamekusanyika walilazimika kutimua mbio.

Watu walioshuhudia tukio lile wanasema viongozi hao akiwamo Mbowe na mwenzake Lissu walikimbilia kwenye magari yao. Lema alilazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe, (kitimoto) kwenye maeneo ya Kaloleni.

Kabla ya polisi kurusha bomu mahali alipokuwapo Lema, mbunge huyo alisikika akisema:

“Jaribuni kuvumilia, tunajaribu kuwasiliana Serikali ya Mkoa, ili watupe kibali cha kuleta miili ya wapendwa wetu hapa, kuweni wastaarabu kwa sababu mbele yetu kuna wana usalama ambao wanalinda amani, ingawa kufa ni kufa tu, wenzetu wameshakufa na sisi ipo siku tutakufa, lakini kila anayetangulia lazima tumzike kwa heshima zote.”

Kauli hiyo iliwachefua polisi ambao walishatangaza amri ya watu kutawanyika katika viwanja hivyo na kwamba hakutakuwa na suala la kuaga miili ya watu hao katika eneo hilo. Ghasia hizo zilisababisha kusimama kwa shughuli za biashara na kijamii kwa muda jijini Arusha huku watu waliokuwa katika nyumba zilizokuwa karibu na maeneo yalikorushwa mabomu wakilazimika kutoka nje kupata hewa safi baada ya nyumba hizo kujaa hewa ya mabomu.

Polisi waliokuwa wakirusha mabomu waliwakimbiza wananchi hadi maeneo ya Sakina huku wakiendelea kufyatua mabomu kila walipoona mkusanyiko wa watu.

Katika eneo la Kaloleni , mkabala na Ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo baadhi ya wafuasi wa Chadema walichoma matairi barabarani na kusababisha ifungwe. Pia walichoma matairi katika eneo la Mianzini

Katika eneo la Tanki la Maji , Barabara ya kwenda Moshi, baadhi ya wafuasi wa Chadema walipanga mawe barabarani na kusababisha msongamano wa magari.

Katikati ya jijini Arusha barabara zilikuwa hazipitiki kutokana na nyingine kufungwa na kusababisha usumbufu mkubwa.

Waandishi nao matatani

Katika vurugu hizo, baadhi ya waandishi wa habari walishambuliwa na polisi. Hao ni pamoja na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la The Citizen, Zephania Ubwani ambaye kabla ya kuchomoka katika mikono ya askari, alikuwa akiwaonyesha kitambulisho chake cha kazi.

Hata hivyo, askari hao walimtishia kumtandika na kisha kumwambia aondoke katika eneo hilo kwa kuwa haijalishi yeye ni nani.

Mwingine ni mwandishi wa gazeti la Nipashe, Cnythia Mwilolezi ambaye alilazimika kuacha viatu na vitendea kazi vyake katika Uwanja wa Soweto na kukimbilia kwenye moja ya nyumba zilizopo jirani na eneo la tukio.

Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, Moses Kilyinga alipigwa na polisi baada ya kuonekana akichukua maelezo.

Kilyinga ambaye alishambuliwa na askari hao alisema mara baada ya askari hao kumkamata, alijitambulisha lakini hawakumwelewa na wakaendelea kumchapa kabla ya kufanikiwa kuchomoka.

Polisi wavamia hospitali

Wakati baadhi ya majeruhi wakidai kushuhudia polisi wakiwapiga risasi watu waliokuwa wakimkimbiza mtu aliyerusha bomu katika tukio la Jumamosi, askari hao juzi walifika katika Hospitali ya Seliani saa mbili usiku wakitaka kumchukua mmoja wa majeruhi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo. Hata hivyo, hawakufanikiwa baada ya mgonjwa kutokomea kusikojulikana baada ya kupata taarifa za kutaka kuhusishwa na tukio hilo.

Ingawa si polisi wala Chadema waliokuwa tayari kumtaja mgonjwa huyo, inaelezwa kwamba majeruhi anayesakwa ni Abdallah Alila aliyekaririwa na vyombo vya habari jana na juzi akidai kumshuhudia aliyerusha boma akiondoka kwenye moja ya magari ya polisi.

Hata hivyo, Kamishna Chagonja jana alisema kwamba jeshi lake linapenda kushirikiana na raia kupata taarifa na si kutumia nguvu katika kukusanya ushahidi wake.

Mwananchi

BEYONCE AWAPONGEZA KIM KARDASHIAN AND KANYE WEST KWA KUPATA MTOTO, CHEKI ALICHOSEMA

New mom Kim Kardashian spent another day in the hospital Monday and got a cyber shoutout from Queen Bey.
Beyoncé posted a heartfelt message to the reality TV star, 32, and Kanye West, 36, after the couple had their baby girl in Los Angeles Saturday. “Congratulations Kim & Kanye,” she wrote on her website. “Enjoy this beautiful moment together.”

Vurugu Arusha; Wabunge Arfi, Lissu, Akunaay Watiwa Mbaroni

Vurugu Arusha; Wabunge Arfi, Lissu, Akunaay Watiwa Mbaroni
WABUNGE wanne wa Chadema, Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu) wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na mkusanyiko usio halali kwenye Uwanja wa Soweto jana.
Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jana kwamba pamoja na wabunge hao pia wamewakamata watu wapatao 60 kutokana na vurugu zilizozuka jana baada ya Polisi kuwatawanya kwenye uwanja huo waliokuwa wamekusanyika kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea kwenye uwanja huohuo, Jumamosi iliyopita.
Mbali ya viongozi hao, alisema wanawasaka Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
“Tunawasaka wabunge ili tuwajumuishe na watu hawa kwa kosa la kuhusika na mkusanyiko usiokuwa halali. Hadi sasa tumefanikiwa kulinasa gari la Mbowe,” alisema Chagonja.
Pia kamatakamata hiyo imemkumba Mpigapicha wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Ashraf Bakari. Polisi walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya waombolezaji hao.
Awali, Kamishna Chagonja alisema jana asubuhi kuwa wamelazimika kuzuia viwanja hivyo kutumika baada ya wamiliki wake, AICC kuzuia shughuli za Chadema kwenye eneo lao. Kamishna Chagonja aliwaonyesha waandishi wa habari barua aliyosema imeandikwa na uongozi wa AICC kuzua Chadema kuendelea kuutumia Uwanja wa Soweto.
Mabomu yarindima
Dalili za kuzuka kwa vurugu zilianza kuonekana asubuhi baada ya polisi kuzingira uwanja huo na kuzuia watu waliokuwa wameanza kufurika katika eneo hilo kuanzia saa moja kuingia kwa ajili ya maombolezo.
Wakati Polisi wakiwa uwanjani, wananchi walijaa nje ya uwanja na kuonekana kama wamewazingira.
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe waliwasili uwanja hapo yapata saa nane mchana na kukuta zuio hilo na kuanza kuzungumza na wananchi ingawa FFU walikuwa wakiwataka watu kutawanyika. Mabomu yalianza kurindima wakati Arfi aliposimama na kuwahimiza wananchi kuelekea Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuaga miili ya marehemu.
“Tuna muda mfupi sana wa kuzungumza hapa, tunaomba wote tuelekee Hospitali ya Mount Meru kuaga miili ya marehemu kwa sababu uwanja huu umezuiwa na polisi,” alisema Arfi kabla ya kukatishwa na milipuko ya mabomu.
Awali, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema alitoa msimamo wa chama hicho kuwa Mwenyekiti wao, Mbowe na Lema hawatatoa ushahidi wa tukio la bomu wala kujisalimisha polisi kwa sababu hawana imani na jeshi hilo.
“Namtaka Chagonja atangulie mahakamani, tutakutana hukohuko. Mbowe na Lema hawatatoa ushahidi wala kujisalimisha polisi…” alisema Lissu na kuongeza:
“Kisheria haiwezekani polisi ambao ndiyo watuhumiwa ndiyo wadai kukabidhiwa ushahidi ili wauharibu.”
Mapema Kamishna Chagonja aliwataka Mbowe na Lema kutoa ushahidi wa polisi kuhusika na tukio la kurusha bomu kwenye mkutano wa Chadema la sivyo polisi watatumia sheria kuwalazimisha kufanya hivyo.
Hekaheka
Baada ya polisi kuanza kutupa mabomu saa 8.45 mchana, wabunge, viongozi waandamizi wa Chadema na watu waliokuwa wamekusanyika walilazimika kutimua mbio.
Watu walioshuhudia tukio lile wanasema viongozi hao akiwamo Mbowe na mwenzake Lissu walikimbilia kwenye magari yao. Lema alilazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe, (kitimoto) kwenye maeneo ya Kaloleni. Kabla ya polisi kurusha bomu mahali alipokuwapo Lema, mbunge huyo alisikika akisema:
“Jaribuni kuvumilia, tunajaribu kuwasiliana Serikali ya Mkoa, ili watupe kibali cha kuleta miili ya wapendwa wetu hapa, kuweni wastaarabu kwa sababu mbele yetu kuna wana usalama ambao wanalinda amani, ingawa kufa ni kufa tu, wenzetu wameshakufa na sisi ipo siku tutakufa, lakini kila anayetangulia lazima tumzike kwa heshima zote.”
Kauli hiyo iliwachefua polisi ambao walishatangaza amri ya watu kutawanyika katika viwanja hivyo na kwamba hakutakuwa na suala la kuaga miili ya watu hao katika eneo hilo. Ghasia hizo zilisababisha kusimama kwa shughuli za biashara na kijamii kwa muda jijini Arusha huku watu waliokuwa katika nyumba zilizokuwa karibu na maeneo yalikorushwa mabomu wakilazimika kutoka nje kupata hewa safi baada ya nyumba hizo kujaa hewa ya mabomu.
Polisi waliokuwa wakirusha mabomu waliwakimbiza wananchi hadi maeneo ya Sakina huku wakiendelea kufyatua mabomu kila walipoona mkusanyiko wa watu. Katika eneo la Kaloleni, mkabala na Ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo baadhi ya wafuasi wa Chadema walichoma matairi barabarani na kusababisha ifungwe. Pia walichoma matairi katika eneo la Mianzini.
Katika eneo la Tanki la Maji, Barabara ya kwenda Moshi, baadhi ya wafuasi wa Chadema walipanga mawe barabarani na kusababisha msongamano wa magari. Katikati ya jijini Arusha barabara zilikuwa hazipitiki kutokana na nyingine kufungwa na kusababisha usumbufu mkubwa.
Waandishi nao matatani
Katika vurugu hizo, baadhi ya waandishi wa habari walishambuliwa na polisi. Hao ni pamoja na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti dada la The Citizen, Zephania Ubwani ambaye kabla ya kuchomoka katika mikono ya askari, alikuwa akiwaonyesha kitambulisho chake cha kazi.
Hata hivyo, askari hao walimtishia kumtandika na kisha kumwambia aondoke katika eneo hilo kwa kuwa haijalishi yeye ni nani. Mwingine ni mwandishi wa gazeti la Nipashe, Cnythia Mwilolezi ambaye alilazimika kuacha viatu na vitendea kazi vyake katika Uwanja wa Soweto na kukimbilia kwenye moja ya nyumba zilizopo jirani na eneo la tukio.
Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, Moses Kilyinga alipigwa na polisi baada ya kuonekana akichukua maelezo. Kilyinga ambaye alishambuliwa na askari hao alisema mara baada ya askari hao kumkamata, alijitambulisha lakini hawakumwelewa na wakaendelea kumchapa kabla ya kufanikiwa kuchomoka.
Polisi wavamia hospitali
Wakati baadhi ya majeruhi wakidai kushuhudia polisi wakiwapiga risasi watu waliokuwa wakimkimbiza mtu aliyerusha bomu katika tukio la Jumamosi, askari hao juzi walifika katika Hospitali ya Seliani saa mbili usiku wakitaka kumchukua mmoja wa majeruhi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo. Hata hivyo, hawakufanikiwa baada ya mgonjwa kutokomea kusikojulikana baada ya kupata taarifa za kutaka kuhusishwa na tukio hilo.
Ingawa si polisi wala Chadema waliokuwa tayari kumtaja mgonjwa huyo, inaelezwa kwamba majeruhi anayesakwa ni Abdallah Alila aliyekaririwa na vyombo vya habari jana na juzi akidai kumshuhudia aliyerusha boma akiondoka kwenye moja ya magari ya polisi.
Hata hivyo, Kamishna Chagonja jana alisema kwamba jeshi lake linapenda kushirikiana na raia kupata taarifa na si kutumia nguvu katika kukusanya ushahidi wake.
CHANZO: www.mwananchi.co.tz

Monday, June 17, 2013

PICHA YA MBUNGE WA ARUMERU JOSHUA NASARIA AKIWA AMELAZWA HOSPITALI

Mbunge Nassari anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Selian Arusha baada ya kushambuliwa vikali na watu wenye marungu,sime ambapo ameumia kifua, shingo na Mgongo....alijinasua hapo baada ya kuwachomoka na kuonyesha silaha nakuweza kuondoka eneo hilo.

CHEKI TUZO ZA BONGO MOVIE 2012-13 ZILIVYOKUWA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki, akimpa tuzo msanii bora wa kiume katika tasnia ya filamu nchini, Jacob Steven 'JB' wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudhuriwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza Steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.

Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji.

Pazia la Tuzo za Steps Bongo Movie Awards likiwa wazi baada ya kufunguliwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia Makame Mbawala.

Msanii Stive Nyerere akipokea Tuzo.

Msanii Nice Mohamedi 'Mtunis' akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entatainment tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.

Shilole akitoa burudani stejini.

Mtoto Jenifa akichukua tuzo yake.

Riyama akipokea tuzo.

Msanii Niva akichukua Tuzo ya msanii bora Chipkizi kulia yupo msanii mwenzake Rado.

Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya kuwakabidhi Tuzo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi 'Ray ' wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabizi tuzo Vicent Kigos 'Ray' ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo.

Baazi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabiziwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizozaminiwa na kampuni ya Steps.

---

KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo.

Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampunu hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo.

Baadhi ya washindi ambao walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Stevin Mangendela 'Stive Nyerere', Issa Mussa 'Cloud 112' Mohamed Nurdini 'Chek budi' Nice Mohamed 'Mtunisi' Iren Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike.

Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Stevin 'JB' huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Iren Uwoya na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda 'Jimmy Masta' Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi' Ray' na kampuni yake ya RJ Filamu mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri rakini kwa sasa awapo duniani moja ni kwa Stevin Kanumba, Saidi Kilowoko 'Sajuki' John Stefano, Hussein Ramadhani Mkiety, 'Sharo Milionea' Katika utoaji wa tuzo huzo kulikuwa na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi