Katika habari iliyoripotiwa na blogs
na magazeti kadhaa ya udaku kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo zilisema
kuwa chanzo ni vitendo vya mwanadada wema Sepetu “kumbania” Kajala
kwenye dili anzopata za kucheza filamu na hasahasa kumkosesha dili ya
kwenda china kufanya filamu aliyoalikwa na watanzania waishio nchini
humo.
Bongomovies.com tuliamua kuwatafuta
hewani wasanii hawa ili tuweze kupata ukweli wa jambo hili na mwanadada
Kajala alikuwa wa kwanza kupokea simu na alikanusha vikali habari hizo
na kuwashangaa wanaoziandika wanazipata wapi.
“Unajua mi nashangaa sana watu
wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi
kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa sijui
nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza
kabla ya kuandika” Alisema kajala
Alipoulizwa kuhusu ukaribu wake mpya na wolper alisema
“Wolper nimekutana naye kwenye party
ndo tukaamua kupiga picha, au siku hizi sitakiwi kupiga picha na mtu
mwingine zaidi ya wema? Wolper ni rafiki yangu” Alisisitiza Kajala
Tulipojaribu kumtafuta wema simu yake
ilikuwa haipokelewi na baadaye ilipokelewa na alisema yuko location
anatengeneza filamu na mwigizaji Rado hivyo tumtafute baadaye.
Credits;Zeddylicious
0 comments:
Post a Comment