Facebook
Facebook
You must log in first.
:forum-110833362/smallform/0:
Need a Facebook account?
Help Center
English (US) · বাংলা · हिन्दी · More…
Facebook ©2012

Sunday, November 24, 2013

Kapuya akimbia nchi


SIKU moja baada ya binti anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kufungua jalada polisi dhidi yake, inadaiwa mbunge huyo ametoweka nchini...
 
Vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na mbunge huyo, vinadai kuwa amesafiri juzi kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.
 
Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini Sweden miezi miwili hadi mitatu.
 
Hata hivyo haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kumtuliza na upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.
 
Wakati Profesa Kapuya anakimbilia nje ya nchi, tayari alishafunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi.
 
Mtoa taarifa wetu anasema muda mchache baada ya Kapuya kushindwa kumshawishi binti huyo asimfungulie kesi ya ubakaji, wala kuogopa vitisho vya kuuawa, au kupokea pesa kiasi chochote aondoke nchini, Kapuya mwenyewe alipanga safari ya dharura na kwenda nje ya nchi.
 
Tanzania Daima  lilifanya juhudi za kuwasiliana na ofisi ya Bunge kujua kama wana taarifa zozote za kuondoka kwa mbunge huyo kwenda nje ya nchi na kujua ni sababu zipi hasa zimempeleka huko, lakini simu ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai ilikuwa inaita bila kupokelewa.
 
Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila naye hakupatikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) hakuujibu.
 
Hata hivyo, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu ambayo Kapuya ni mjumbe wake haina safari ya Sweden.
 
Tangu Tanzania Daima lianze kuandika tuhuma hizi nzito, kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi.
 
Harakati za kufungua jalada dhidi ya Kapuya zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.
 
Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.
 
Polisi wanena
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake zitathibitika.
 
Alisema Jeshi la Polisi lina mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
“Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na kurejeshwa kwao.
 
“Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana na hatufanyi kazi kinyume na taratibu zetu,” alisema.
 
Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya huku akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake.
 
Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.
 
“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.

Source: Tanzania Daima

Thursday, November 21, 2013

Sababu za Adan Rage kusimamishwa Adan Rage wazijua?Zisome hapa..Uongozi umezifafanua zaidi.

Jana uongozi wa klabu ya Simba ulitangaza kumsimamisha mwenyekiti wake Ismail Aden Rage.
Maamuzi hayo yalitokana na kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika hapo juzi,
Hizi ni Miongoni mwa sababu zilizotolewa kwenye mkutano wa waandishi wa habari zilizopelekea kusimamishwa kwa Mheshimiwa Rage.
Mkataba na AZAM  TV
Rage alisaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya kipindi ya cha Simba TV bila kuishirikisha kamati ya utendaji.
Wakati Rage anasaini mkataba na Azam TV tayari klabu ya Simba ilikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho kuingia mkataba na kampuni ya ZUKU kwa ajili kipindi cha Simba TV uliokuwa na thamani ya dola za kimarekani 300,000 kwa mwaka.
Kampuni ya ZUKU ilipokuwa kwenye majadiliano na viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga jijini Nairobi, kwenye mkutano huo Simba iliwakilishwa na Mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph Itang’are maarufu kama mzee Kinesi pamoja na mwanachama Evans Aveva wakati Yanga iliwakilishwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga na Francis Kifukwe,viongozi hao Simba Ghafla walisikia Rage kasaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya Simba TV.
Sakata la uhamisho wa Emmaanuel Okwi.
Mheshimiwa Rage ndiye aliyesimamia uhamisho wa mchezaji Okwi on CREDIT bila kuishirikisha kamati ya utendaji,matokeo yake klabu hiyo mpaka leo imeshindwa kupata pesa ya uhamisho wa mchezaji huyo.
.
Kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji.
Sababu nyingine iliyoelezwa ni kitendo chake cha kushindwa kuitisha vikao vya kamati ya utendaji, Kuendesha klabu na kufanya maamuzi binafsi bila ya kushirikisha kamati hiyo ya utendaji ambayo ilichaguliwa na wanachama
Strategic plan ( Mpango mkakati )
Hivi karibuni klabu ya Simba ilizindua mchakato wa kutengeneza mpango mkakati (Strategic Plan) lakini cha kushangaza mwenyekiti amekuwa hataki kuona mpango huo ukifanikiwa.
Mkutano mkuu wa katiba

Kushindwa kuitisha mkutano wa marekebisho ya katiba,kuchukua maamuzi binafsi ya kuhairisha mkutano maalumu wa katiba uliotakiwa kufanyika Novemba, mwaka huu.

Vichwa vya habari vya magazeti ya leo Alhamisi tarehe 21 November 2013

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.


                           Source;millardayo.com

BABU SEYA KULIA AU KUCHEKA LEO?

MAHAKAMA ya Rufani leo inatarajia kutoa uamuzi wa ama kulikubali au kulikataa ombi la marejeo lililowasilishwa na mwanamuziki wa dansi nchini, Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae, Papi Kocha ‘Mtoto wa Mfalme’, ambao waliomba mahakama hiyo ifanyie marejeo hukumu ya kifungo cha maisha iliyoitoa Februari 2010, kwa kuwa ina dosari za kisheria na kuwaachia huru.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa mahakama iliyotolewa kwa mawakili wa pande zote mbili, mahakama imemtaka Babu Seya na mwanae pamoja na mawakili wa pande zote kufika leo mahakamani ili wapokee uamuzi wa maombi hayo.

Oktoba 30 mwaka huu, jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk, walisikiliza ombi hilo lililowasilishwa mahakamani hapo na wakili wa waomba rufani, Mabere Marando.

Wakili Marando alidai kwa mujibu wa kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009  inatoa mamlaka kwa Mahakama ya Rufaa kufanya mapitio  ya hukumu inazozitoa,  hivyo wateja wake wamewasilisha ombi hilo kwa sababu wanaamini  mahakama ilikosea kisheria katika hukumu yake Februari 2010.

“Waheshimiwa majaji, kwa sababu jopo lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi  kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi wa watoto waliodai walitendewa vibaya na waomba rufaa (Babu Seya na Papii) na sheria za nchi zinasema endapo mahakama itabaini kuwa mahakama ya chini ilikiuka taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto wadogo, basi ushahidi ule wa watoto wadogo uliotumika katika mahakama ya chini kuwatia hatiani washitakiwa unafutwa na waomba rufaa au washitakiwa wanaachiwa.

“Nafahamu ni kazi ngumu kuwashawishi nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februari 2010, ambapo uliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa utetezi huo wa kisheria niliouainisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na hoja yangu kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi wa watoto wadogo, naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria na leo naiomba mahakama iwaachie huru wateja wangu,” alidai Marando.

Mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP), Angaza Mwipopo, Jackson Mlati, Imaculata Banzi na Joseph Pande, waliomba mahakama itupilie mbali ombi hilo, kwa kuwa sababu zote alizozitoa alizieleza wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamuliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februari mwaka 2010.

Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari, angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na si ombi lake kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu hiyo ambayo anadai ina dosari.

Source;TANZANIA DAIMA